Na
Mahmoud Zubeiry, Kampala
BIASHARA
imeisha. Azam FC imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000
kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini mkataba wa miaka miwili,
utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani 4,000 kwa mwezi huku naye
akilipwa dola 50,000 za kusaini.Kwa hisani ya Bongostaz
Blog
Awali,
Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola
100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema utambana
mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa
Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker
Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari
kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya
michuano ya klabu Afrika.
Azam
FC imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa kwa ujumla katika maamuzi
ya kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa mkopo. “Hii timu
(Merreikh) kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika,
maana yake huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja kuisaidia zaidi
Tanzania katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa
kuhusu Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu hiyo, kiongozi huyo alisema wao
walimtoa kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa Msimbazi hadi Mei 31, mwakani na
mkataba wao ndio unasema hivyo.
“Sisi
tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31 na wakatupa Sh. Milioni 25,
ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota, lakini huyu mchezaji ni mali
yetu na hata TFF wanatambua hilo, na tumekwishamuuza
Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa
kuhusu Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa, alisema; “We uliona wapi dunia
nzima timu inapewa mchezaji kwa mkopo halafu inamsainisha mkataba? Simba lazima
ifike wakati waache kurudia makosa, haya ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema
kiongozi huyo wa Azam.
Katika
kukamilisha mauzo ya mchezaji huyo, kiongozi wa Marreikh akiwa Dar es Salaam
mbele ya viongozi wa TFF na Azam, alipigiwa simu Ngassa aliye hapa Kampala,
Uganda na kuhusishwa katika dili hilo, naye akakubali ndipo mambo
yakamalizwa.
Aidha,
Azam wameomba TFF ihakikishe kunakuwa na ulinzi katika kambi ya timu ya taifa
mjini hapa, ili Simba wasimfanyie vurugu Ngassa na kumvuruga kisaIkolojia,
wakati ndiyE tegemeo la timu katika kampeni ya kutwaa Kombe la Challenge mwaka
huu mjiini hapa.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe
akizungumza kutoka Dar es Salaam, alisema kwamba watawapeleka mahakamani Azam
kwa kitendo cha kumuuza mchezaji wao kinyume cha sheria.
“Haiwezekani
wamuuze wao, wakati wao walituuzia huyu mchezaji na sisi tuna mkataba ambao
tulisaini nao, hii ni kinyume cha sheria na sisi tutawapeleka
mahakamani,”alisema Hans Poppe ambaye anatua kesho mjini
hapa.
Azam
walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na
kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu
Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS
Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya
hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam
kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara
nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza
kinazi.
Ilielezwa
kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa
baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji
huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni
30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa
gari.
KAULI YA AZAM FC JUU YA KUUZWA KWA NGASA
Post a Comment