Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NAPE AMPA ANGALIZO DKT. SLAA

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye
--
Na Mwandishi Wetu-Gazeti la Majira

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye, amempongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kukiri kumiliki kadi ya chama chao hadi sasa.

Alisema Dkt. Slaa ameanza kujifunza kusema ukweli baada ya kutambua uongo haulipi kwani kitendo cha kukiri kumiliki kadi ya CCM ni cha kiungwana hivyo anastahili pongezi.

Bw. Nnauye aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya Dkt. Slaa kujibu tuhuma zake kuwa, wapo baadhi ya vigogo wa CHADEMA ambao wanamiliki kadi za CCM na wanazilipia hadi sasa.

“Dkt. Slaa amekiri katika vyombo vya habari kuwa anamiliki kadi ya CCM hadi sasa akidai anaitunza kama kumbukumbu muhimu hivyo ni vyema akawaeleza Watanzania kadi yake ameilipia hadi lini na aache kuwadanganya wenzake warudishe kadi za chama tawala wakati yeye ameendelea kuwa nayo,” alisema.

Bw. Nnauye amekiri kumheshimu sana Dkt. Slaa kama babu yake na alishtuka sana kusikia Katibu Mkuu huyo anawatuhumu baadhi ya viongozi wa CHADEMA na kudai ni mamluki wa CCM wakati yeye ni namba moja kwani anaowatuhumu hawana kadi za chama hicho.

“Nilimsikia Dkt. Slaa akiwatuhumu baadhi ya viongozi ndani ya chama chao kuwa ni mamluki wa CCM, hili linawasaidiaje Watanzania maskini.

“Kitendo hiki kimethibitisha upeo mdogo alionao katika kufikiri, huyu ni kiongozi mkubwa ambaye namuheshimu lakini anapaswa kujua yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake,” alisema Bw. Nnauye na kuongeza;

“Viongozi wa aina yake ni janga kwa Taifa letu, usipokuwa mwaminifu kwa kidogo, huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top