Mambo makubwa yamefanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba usiku huu jijini Mwanza ambapo Mwanamuziki Gwiji la
miondoko ya bolingo, Barani Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kofii
Olomide akiwa na kundi lake amepagawisha mashabiki wa muziki wake katika tamasha
la Tusker Carnival .
Mwanamuziki Kofii Olomide amefanya mambo makubwa
kama alivyoshusha burudani jana kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam,
Watu mbalimbali wamiminika kwenye uwanja wa CCM Kirumba ili kumuona mwanamuziki
huyo (pichani juu) akiwa na first lady wa bendi hiyo mwanamama Cindy
aliyetambulishwa kwa mashabiki wa jijini Mwanza.
Kofii Olomide akiimba huku akiwa
amezungukwa na wanenguaji wake
Mwanamuziki Kofii Olomide akipanda jukwaani huku
akisinddikizwa na waimbaji wake.
Mwanamuziki Cindy katikati Mwimbaji mahili wa
mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani kalba ya Kofii kupanda
jukwaani.
Kazi iko hapa kama wanavyoonekana wanenguaji hao
wakicheza kwa staili mpya.
Hii ilichezwa kwa kwenda mbele na kurudi nyuma huku
wakiwa wameshikana.
Palikuwa hapatoshi kwa shoo
kabambe.
Ili mradi burudani iliyopangika
kutoka kwa wanenguaji hao
Kutoka kulia ni Ephraim Mafuru, Anitha Msangi
Maurice Njowoka na Patrick Kisaka kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakishoo
love kwa picha.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim
Mafuru kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakiwa katika
picha ya pamoja
Wadau kutoka Miss Tanzania wakiwa katika onesho
hilo.
Rachel wa THT akicheza na mmoja wa wanenguaji wa
mwanamuziki Kofii Olomide.
Kofii Olomide akimpongeza msanii
Rachel wa THT baada ya kuonyesha uwezo wake katika kuimba kwenye onesho
hilo.
Waimbaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakiimba kwa hisia
katika enesho hilo.
Rapawa mwanamuziki Kofoo Olomide anayejulikana kwa
jina la Computar akighani jukwaani huku wanenguaji wa kiume wakiingia
jukwaani.
Jukwaani ni Recho wa kundi la THT kutoka jijini Dar es
salaam akinendelea kutoa burudani jukwaani
H. Baba
akifanya vitu vyake mbelea ya mashabiki wa jijini Mwanza wakati aktoa burudani
ya utangulizi kabla ya mwanamuziki Kofii Olomide Kupanda
jukwaani.
Pepe Kale wa Mwanza naye akaifanya
mambo makubwa na kukubalika na umati wa mashabiki waliohudhuria katika onesho
hilo.
Wasanii wa Kundi la THT
likitumbuiza katika onesho hilo.
Bendi ya Hill Way ya Mwanza
ikitumbuiza katika utangulizi
Kundi la Hill Way Band likifanya vitu
vyake jukwaani katika utanguliziwa urudani za tamasha la Tusker Carnival kabla
ya mwanamuziki Kofii Olomide kupanda jukwaani.
Mashabiki wakiwa wameanza
kumiminika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mashabiki wakiwa kwenye uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakisubiri kuona burudani ya Kofii
Olomide.
Haya ni maeneo maalum
yaliyotengwa kwa ajili ya kujipatia bia yako ya Tusker Lager na vinywaji vingine
vinavyotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
Haya ni maeneo maalum
yaliyotengwa kwa ajili ya kujipatia bia yako ya Tusker Lager na vinywaji vingine
vinavyotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti. PICHA ZOTE KWA HISANI YA
FULLSHANGE.COM
Post a Comment