Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania,
Lawrence Mafuru (kushoto) na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Lindi, Thomas Sowani wakikata utepe kuzindua jengo la maktaba ya Shule ya
Sekondari Angaza lililokarabatiwa
na NBC katika hafla iliyofanyika Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Meneja wa
NBC Lindi, Godfrey Chilewa , Mkuu
wa Sekondari ya Angaza, Upendo Muro, Mkurugenzi wa Read International Tanzania, Montse Pejuan na Meneja
Mahusiano ya Kijamii wa NBC, Robi
Matiko-Simba. NBC imetumia jumla ya shs milioni 70 kukarabati shule sita za sekondari katika mikoa
tofauti nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania,
Lawrence Mafuru (katikati) akitoa
maelekezo kuhusu somo la hisabati kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Angaza, Zainab
Chikira (kushoto)n na Bahati Adam
(kulia) katika hafla ya uzinduzi wa jengo la maktaba ya shule hiyo lililokarabatiwa na NBC, hafla
iliyofanyika shuleni hapo, Mkoani
Lindi mwishoni mwa wiki
Meneja Mahusiano ya Kijamii wa NBC, Robi
Matiko-Simba (katikati), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Angaza, katika hafla ya
uzinduzi wa jengo la maktaba ya shule hiyo lililokarabatiwa na NBC, hafla iliyofanyika
shuleni hapo, Mkoani Lindi mwishoni
mwa wiki.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Benki ya NBC
Tanzania, Jane Dogani (kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (katikati) katika hafla ya uzinduzi wa
jengo la maktaba ya
shule hiyo
lililokarabatiwa na NBC, hafla iliyofanyika shuleni hapo,Mkoani Lindi mwishoni
mwa wiki. Wengine ni maofisa wa NBC, walimu na viongozi wa Mkoa wa
Lindi.
Meneja wa NBC Tawi la Lindi, Godfrey Chilewa
(kushoto), akizungumza na baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Angaza, katika hafla ya uzinduzi wa jengo la maktaba ya
shule hiyo lililokarabatiwa na NBC,
hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. NBC imetumia jumla ya shs
milioni 70 kukarabati shule
sita za sekondari katika maeneo tofauti nchini.
Post a Comment