Askofu Msaidi wa Jimbo Kuu la
Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa (katikati) akiongoza ibada ya mkesha wa Sikuu
ya Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam
juzi. Kushoto ni Paroko wa kanisa hilo, Padri, Joseph Mosha. (Picha na Habari
Mseto Blog)
Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa mahubiri wakati
wa ibada ya Krismasi leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa baraka kwa
waumini wa Usharika wa Azania Front baada ya ibada ya Krismasi
Sehemu ya waumini wa Kanisa
Katoliki Parokia mpya ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi wakifuatilia sehemu ya ibada
ya Krisamsi iliyokuwa ikiendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, Dar es Salaam leo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la
Dar es salaam Muadhama Polycarp Kadinali Pengo akipokea michango mbalimbali ya
fedha kutoka kwa viongozi wa jumuiya za kikristo katika jimbo la segerea, dar es
salaam alipokwenda kuongoza ibada ya Krismasi sambamba na uzinduzi wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi, Dar es Salaam leo.
Post a Comment