WAKRISTO duniani kote
leo wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi.
Maelfu ya watu
wamekusanyika katika mji wa Bethlehem kwenye Mamlaka ya Wapalestina kusheherekea
sikukuu hiyo.
Mji huo unaaminika kuwa ndiko pahala alikozaliwa masiha
yesu kristo.
Misa kubwa ilifanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kanisa
kongwe mjini humo na kuhudhuriwa na Rais Mahmoud Abbas.
Padri Mkuu wa
kanisa Katoliki kwenye eneo la Mashariki ya Kati, Fuad Twal ndiye aliyeongoza
misa hiyo na kusema kuwa wanasheherekea si tu kuzaliwa kwa yesu kristo bali pia
kuzaliwa kwa taifa la Palestina.
Katika kuadhimisha siku hii huko Rome
ambako ndiko makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedict wa
16 aliongoza misa kubwa usiku wa kuamkia leo.
Ujumbe wa Baba Mtakatifu
Benedict wa 16
Baba Mtakatifu Benedict
wa 16 akiongoza ibada.
Ujumbe wa Baba Mtakatifu
kwenye sikukuu hii ni kuwepo kwa amani kwenye eneo la mashariki ya
kati.
Amewataka pia watu wote duniani kumpa mungu nafasi kwenye maisha
yao ya kila siku.
Katika misa hiyo maalumu kwa ajili ya Krismas ambayo
inawaunganisha Wakatoliki wapatao bilioni 1.2 duniani kote, Baba Mtakatifu
ameonya pia kuhusu vitendo vya ubaguzi wa kidini.
Maelfu ya watu
walimiminika katika viunga vya kanisa la Mtakatifu Peter mjini Vatican kwa ajili
ya ibada hiyo ya takribani masaa mawili ambayo ilionyesha pia na vyombo vya
habari mbalimbali duniani kote.
Akiwa amshiba mslaba wake wa dhahabu na
kuvalia mavazi yaliyopambwa kwa rangi ya dhahabu Baba Mtakatifu mwenye umri wa
miaka 85 alionekana mwenye furaha.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki
duniani alisema " wacha tuombe mungu kwa ajili ya Waisraeli na Wapalestina ili
waishi maisha ya amani ya mungu mmoja na uhuru".
Ameiombea pia mizozo
inayoendelea katika nchi za Syria, Lebanon, Iraq na majirani zao kwenye eneo la
mashariki ya kati.
Baba Mtakatifu kutoa Baraka
za Krismas
Kijana wa Afrika Kusini
akiuza mapambo ya Krismas.
Aliomba akisema kuwa
wakristu kwenye eneo hilo ambalo imani yao ilizaliwa wapate uwezo wa kuendelea
kuishi huko, na kwamba wakristu na waislamu wajenge mataifa yao kwa ushirikiano
kwa amani ya mungu.
Kiongozi huyo mzaliwa wa Ujerumani amepinga suala la
kusema kuwa dini ndizo zinafaa kulaumiwa kwa machafuko yanayoendelea kwenye nchi
mbalimbali duniani, ingawa alikubali kuwa dini inaweza baadhi ya wakati
ikatumika vibaya.
Akaonya " lazima tuwe waangalifu kwa maneno haya ya
upotoshaji dhidi ya utukufu".
Hii leo kiongozi huyo atatoa baraka za siku
hii majira ya mchana katika lugha mbalimbali kwa ajili ya miji na
taifa.
Wiki iliypita kiongozi huyo alipaza sauti kupinga ndoa za jinsia
moja akisema mahusiano hayo yanakwenda kinyume na maumbile ya mwanadamu ambayo
ni kuwepo baba. mama na watoto.
Krismas hii inakuja wakati kanisa
katoliki likiwa limekumbwa na mkasa wa kuvuja kwa taarifa za ndani kwenye vyombo
vya habari kuhusu masuala ya rushwa, mzozo wa madaraka.

WAKRISTO duniani kote
leo wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi.
Mji huo unaaminika kuwa ndiko pahala alikozaliwa masiha yesu kristo.
Misa kubwa ilifanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kanisa kongwe mjini humo na kuhudhuriwa na Rais Mahmoud Abbas.
Padri Mkuu wa kanisa Katoliki kwenye eneo la Mashariki ya Kati, Fuad Twal ndiye aliyeongoza misa hiyo na kusema kuwa wanasheherekea si tu kuzaliwa kwa yesu kristo bali pia kuzaliwa kwa taifa la Palestina.
Katika kuadhimisha siku hii huko Rome ambako ndiko makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedict wa 16 aliongoza misa kubwa usiku wa kuamkia leo.
Ujumbe wa Baba Mtakatifu
Benedict wa 16


Baba Mtakatifu Benedict
wa 16 akiongoza ibada.
Amewataka pia watu wote duniani kumpa mungu nafasi kwenye maisha yao ya kila siku.
Katika misa hiyo maalumu kwa ajili ya Krismas ambayo inawaunganisha Wakatoliki wapatao bilioni 1.2 duniani kote, Baba Mtakatifu ameonya pia kuhusu vitendo vya ubaguzi wa kidini.
Maelfu ya watu walimiminika katika viunga vya kanisa la Mtakatifu Peter mjini Vatican kwa ajili ya ibada hiyo ya takribani masaa mawili ambayo ilionyesha pia na vyombo vya habari mbalimbali duniani kote.
Akiwa amshiba mslaba wake wa dhahabu na kuvalia mavazi yaliyopambwa kwa rangi ya dhahabu Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 85 alionekana mwenye furaha.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani alisema " wacha tuombe mungu kwa ajili ya Waisraeli na Wapalestina ili waishi maisha ya amani ya mungu mmoja na uhuru".
Ameiombea pia mizozo inayoendelea katika nchi za Syria, Lebanon, Iraq na majirani zao kwenye eneo la mashariki ya kati.
Baba Mtakatifu kutoa Baraka
za Krismas

Kijana wa Afrika Kusini
akiuza mapambo ya Krismas.
Kiongozi huyo mzaliwa wa Ujerumani amepinga suala la kusema kuwa dini ndizo zinafaa kulaumiwa kwa machafuko yanayoendelea kwenye nchi mbalimbali duniani, ingawa alikubali kuwa dini inaweza baadhi ya wakati ikatumika vibaya.
Akaonya " lazima tuwe waangalifu kwa maneno haya ya upotoshaji dhidi ya utukufu".
Hii leo kiongozi huyo atatoa baraka za siku hii majira ya mchana katika lugha mbalimbali kwa ajili ya miji na taifa.
Wiki iliypita kiongozi huyo alipaza sauti kupinga ndoa za jinsia moja akisema mahusiano hayo yanakwenda kinyume na maumbile ya mwanadamu ambayo ni kuwepo baba. mama na watoto.
Krismas hii inakuja wakati kanisa katoliki likiwa limekumbwa na mkasa wa kuvuja kwa taarifa za ndani kwenye vyombo vya habari kuhusu masuala ya rushwa, mzozo wa madaraka.
Post a Comment