Christopher
Katongo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa BBC mwaka wa 2012.
Nahodha
huyo wa Zambia mwenye miaka 30 amemshinda Demba Ba, Didier Drogba, Younes
Belhanda na Yahya Toure na kuwa mshindi wa kwanza kutoka Kusini mwa Afrika
katika historia ya mashindano hayo.
Orodha
ya washindani hao ilitengazwa na wataalamu wa soka Afrika, ambao wamezingatia
umahiri wa mchezaji, uwezo wa kiufundi na ushirikiano na wachezaji
wengine.
Na
idadi kubwa ya watu wamepiga kura kupitia njia ya mtandao au ujumbe mfupi huku
asilimia 40 kati yao wakimchagua Katongo, ambaye anachezea timu ya China Henan
Construction.
Katongo
aandikisha rekodi mpya
Huku
wachezaji wote walioorodheshwa katika kinyang'anyiro hicho walikuwa na mwaka
mzuri, wanne kati yao walikuwa wameshinda medali mbali mbali, ni Katongo pekee
ambaye mafanikio yake yamezingatiwa na mashabiki wa mpira
Afrika.
Katongo,
ambaye ni mwanajeshi nchini mwake, alikuwa kivutio pindi alipoiongoza Zambia,
katika michuano ya kombe la Mataifa Bingwa barani Afrika mnamo mwezi wa Februari
mwaka huu.
Alifunga
magoli matatu katika fainali iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea na Gabon na
baadaye kufunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti na kuisadia Zambia
kunyakuwa kombe hilo.
Zambia
iliishindi Ivory Coast kwa 8-7 katika fainali hiyo baada ya timu hizo mbili
kutoshana nguvu baada ya muda wa kawaida na muda wa ziada mjini
Libreville.
KATONGO AFUFUA MATUMAINI YA ZAMBIA KUELEKEA BRAZIL
Kilikuwa ni kipindi kilichojawa na hisia kwa Zambia,
ambayo miaka 19, iliyopita ilipata msiba mkubwa, pale ndege iliyokuwa imebeba
wachezaji wa timu ya taifa ilipoanguka mita 500 tu mbali na Libreville, na kuuwa
wachezaji wote 25 na rubani wake.
Miezi
saba baada ya kuongoza Zambia kushinda kombe hilo, Katongo vile vile amekuwa
nyota wa timu yake ya taifa wakati wa michuano ya kufuzu kwa fainali za mwaka
ujao,wakati alifunga goli la pekee dhidi ya Uganda.
Bao
hilo liliibuka kuwa bao muhimu sana kwa Zambia kwa kuwa ilipoteza mechi
iliyofuatia kwa bao moja kwa bila, lakini ikafuzu kwa fainali za mwaka 2013
zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini baada ya kushinda kwa magoli 9-8 kupitia
mikwaju ya penalti.
MIKAKATI YA KUFUZU KWA KOMBE LA DUNIA
Na
zaidi ya hayo yote, Katongo amechangua pakubwa harakati za kufufua matumaini ya
Zambia ya kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa
2014.
Zambia
ililazwa magoli 2-0 na Sudan mjini Khartoum mwezi Juni, matokeo ambayo hadi
wakati huu hayajathibitishwa, huku uchunguzi ukiendelea kuhusu hatua ya Sudan ya
kumshirikisha mchezaji ambaye hakuwa amesajiliwa.
Wiki moja baada ya mechi hiyo Zambia
ilichuana na Ghana na Katongo kwa mara nyingine ndiye aliyefunga bao la ushindi
na hivyo kuimarisha matumaini yao ya kufuzu.
Ikiwa
Christopher Katongo ataendelea na hali aliyo nayo kwa sasa, huenda akaisaidia
Zambia kuandikisha matokeo mazuri wakati wa michuano ya kuwania kombe la dunia
nchini itakayoandaliwa nchini Brazil miezi kumi na minane ijayo
Post a Comment