Sasa imezinduliwa
rasmi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akikata utepe kuzindua rasmi
taarifa ya hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo
ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kushoto) Mkurugenzi
Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot (wa tatu kulia), Afisa Mwakilishi
wa UNEP Tanzania Clara Makenya (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava ( wa kwanza kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akitoa hotuba wakati wa
uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema
katika Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) uliofanyika
mjini Kampala Julai 2002, ulibaini kuwa ukosefu wa taarifa za hali ya mazingira
katika bara la Afrika ni moja ya sababu zinazochangia mipango duni ya usimamizi
wa shughuli za maendeleo na utekelezaji Mikataba ya Kimataifa ya utunzaji
mazingira.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais Bw. Sazi Salula akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam
akisema Tanzania ni moja ya nchi zinazotekeleza program ya mtandao wa taarifa za
hali ya mazingira yaani “Africa Environmental Information Network (AEIN) chini
ya ufadhili wa Shirika la Mpango wa Mazingira Duniani (UNEP).
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP
nchini Tanzania Phillipe Poinsot akizungumza kabla Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa hajazindua Taarifa ya Hali ya
Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema taarifa hiyo ina mapendekezo
makuu 12 na kutoa wito kwa serikali ya Tanzania kutafakari kila pendekezo
sambamba na kuzitumia taarifa za kimazingira kwa manufaa ya
taifa.
Amesema
kutokana na hali hiyo AMCEN iliiomba UNEP wafadhili program ya Afrika ya Mtandao
wa Hali ya Mazingira (Africa Environmental Information Network) ili kuongeza
uwezo wa nchi za Afrika wa kuwa na Taarifa za Hali ya Mazingira na Mtandao wa
Habari baina ya nchi za Afrika.
Mh. Huvisa
ameweka wazi kuwa taarifa hiyo imekamilika na iko tayari kwa ajili ya
utekelezaji, na kuwa taarifa hiyo imeezea Historia ya jiji la Dar es Salaam,
Jiografia na Fiziolojia yake, suala la uchumi Jamii, Sera, Sheria na Mfumo wa
Utawala Kimazingira, Usimamizi wa Rasilimali ya Ardhi, Rasilimali Maji, Madini
na Nishati, Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira, Uchafuzi wa Mazingira na
Mabadiliko ya Tabianchi
Post a Comment