SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amewataka Waislam nchini kuacha kulalamika kuhusu matumizi ya tarehe na mwaka Wakislam katika shughuli mbalimbali za kijamii.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Alhad, alisema hayo wakati wakuupokea mwaka
mpya (1434), suala la matumizi ya tarehe na mwaka huo si la serikali wala dini
nyingine bali ni la kwao wenyewe.
Alisema waislam wanapaswa
kubadilika kwa kuanza kutumia tarehe hizo, katika shughuli mbalimbali ikiwemo
katika kuandikiana barua ziwe za kidugu, kiofisi na hata katika malipo ya
mishahara.
Alhad alisema
kinachojitokeza katika hilo ni kwamba Waislam wenyewe bado hajaonesha mapenzi ya
kuukubali mwaka wao kutokana na kupenda kutumia kalenda za
miradi.
Aidha, hakuna haja ya
kusherehekea na kuupokea mwaka huo mpya wa Kiislam kila unapofika wakati wenyewe
hawautambui ambapo, ili kutambulika ni lazima kila mwislam ahakikishe anatumia
tarehe na mwaka kwa ajili ya kumbukumbu za shughuli zote zinazogusa maisha
yao.
“Ifike mahala tukubaliane
waislam wote kuwa kila mmoja wetu ni lazima atumie tarehe hizi na asiyefanya
hivyo asiruhusiwe kuhudhuria sherehe za kuupokea mwaka mpya unapoingia”alisema
Alhad.
Alisema utakuta muislam
analalamika kuwa mwaka huo hautumiki huku yeye mwenyewe ukifika nyumbani kwake
amebandika kalenda hizo za miladi, ingawa siyo ukafiri kutumia kalenda hizo kama
inavyodaiwa na baadhi yao.
Katika hatua nyingine,
Alhad aliungana na maombi ya baadhi ya taasisi za dini hiyo kwa serikali kuwa
Siku hiyo ya mwaka mpya wadini hiyo kuwa ya mapunziko kama ilivyo zile za
kalenda ya kawaida iliyozoeleka.
Post a Comment