Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokelewa na
viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani
Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati
wa kanisa hilo,iliyofanyika leo Mkoani humo.
===========
========= =========
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena
kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati
alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika
wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo
lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari.
''tunashuhudia
maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na
ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini
kwetu.
huko
nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi
za serikali kutatua suala hilo''alisema Lowassa.
Lowassa
ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia
yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni
33.2.
Zaidi ya
shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana
katika harambee hiyo.
Kwa
upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake
popote alipokuwa.''Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia
uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako''alisema na kuongeza kuwa
Lowassa ni mtu wa ibada.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu kushoto)
akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi
ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia muda
mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani
usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea ahadi ya
mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa
Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani
Arusha.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka kanisani
hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani
usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Post a Comment