Zoezi la kuhesabu kura lilianza baada ya kumalizika kwa upigaji kura huku matokeo ya awali yakionesha kuelekea kuidhinishwa kwa kura hiyo ya maoni, vimeripoti vyombo vya habari vya nchi hiyo.
Chama cha rais Mohammed Mursi cha Udugu wa Kiislamu pamoja na washirika wao wamefanya kampeni kwa nguvu ili rasimu hiyo ya katiba iidhinishwe, wakidai kuwa ni muhimu kuharakisha hatua za mpito kutoka utawala wa kiimla wa Mubarak.
Upande wa upinzani unasema kuwa katiba hiyo, iliyoandikwa na baraza linalomilikiwa na vyama vinavyoongozwa na makundi ya Kiislamu , inaweza kukandamiza haki za wanawake na za kisiasa na kuwatenga watu wa makundi ya wachache.
“Sipendi mfumo wa Kiislamu udhibiti nchi yangu kwa sababu nafahamu kuwa Mursi ni dikteta, anadhibiti maisha yangu na ya familia yangu. Napendelea uhuru,” Naier al-Guindy, mwenye umri wa miaka 59, ameliambia shirika la habari la dpa katika kituo cha kupigia kura cha Garden City katikati ya mji wa Cairo.
Post a Comment