Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Amzawadia Tuzo Mwandishi Wa New Habari



NA: GLADNESS MUSHI -ARUSHA
MKUU wa Mkoa wa Arusha amemzawadia tuzo ya uandishi bora wa habari za jamii na maendeleo Meru , mwandishi wa habari Mary Mwita wa magazeti ya Mtanzania na Rai ya Kampuni ya New habari (2006) LTD.

Mkuu wa Mkoa huyo ametoa tuzo hiyo ,ikiwa ni ahadi yake ,na agizo alilotoa kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kupeleka jina la Mwandishi wa habari aliyeandika habari bila kupotosha jamii katika Halmashauri hiyo ,na kuweza kumpata Mwandishi huyo .

Mkuu alitoa Tshs 500,000 ikiwa ni tuzo na kiasi cha fedha zilizokabidhiwa kwa wadau wengine mwaka huu waliobainika kuchangia maendeleo ya Meru.

Mkuu huyo alisema kuwa huwezi kutaja maendeleo bila kuhusisha vyombo vya habari na waandishi wa habari ,na kuwa kila Halmashauri inatakiwa kutambua mchango wa maendeleo ya wadau ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari .

Akimpongeza Mwandishi Mary Mwita ,alisema wakati umefika wa waandishi wa habari kuandika habari za kweli bila kupotosha umma ,ikiwa ni kuwawezesha wananchi kujifunza na kupata ujuzi kupitia habari hiyo ,badala ya kuandika habari za uongo .

Mlongo alisema kuwa ni wazi kuwa kila mtu katika jamii akisimama katika nafsi yake kulingana na karama aliyopewa Maendeleo ya haraka yatafikiwa na kuwawezesha wananchi kupunguza kasi ya umaskini katika jamii .

Katika hatua nyingine alipongeza uongozi wa Halmashauri ya Meru kwa kutambua mchango wa maendeleo ya wadau na kutaka Halmashauri nyingine kuiga mfano huo wa kutunikia zawadi wadau waliosaidia maendeleo ya Halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Trisas Kagenzi alisema kuwa zoezi la kuwazawadia wadau ni endelevu ,na kuwa wataendelea kutambua mchango wao kwa kuwa bila ushirikiano na wadau wa maendeleo ,maendeleo yanaweza kuchelewa .

Kagenzi alisema kuwa Mwandishi Mary Mwita ,amekuwa akiandika habari bila kupotosha umma kwa kujituma na kutaka waandishi wengine kuiga mfano wake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top