![]() |
Angelina Jolie |
Muigizaji wa kike Angelina Jolie
aliyetamba sana na action movie ya Mr.&Mrs. Smith amefunguka katika
interview aliyofanya na kituo cha televisheni cha Uingereza ‘4 News’ kwamba
anampango wa kuachana na kazi yake ya uigizaji muda mfupi ujao.
Mshindi huyo wa tuzo za Oscar ambae
yuko busy akiandaa movie yake ‘Maleficent’ anaona wakati umefika sasa anataka
kuachia ngazi kwa sababu mbalimbali hasa sababu za kifamilia na majukumu ya kazi
za nyumbani, “nadhani naelekea kuachana na uigizaji kwa wakati mwanangu anafikia
umri wa miaka 13 hivi, anyway, shunguli nyingi sana za kufanya
nyumbani.”
Angelina Jolie mwenye watoto sita
alikiri kuenjoy kuwa muigizaji na ukizingatia yuko kwenye list ‘A’ ya Hollywood
Stars, “nimekuwa naenjoy sana kuigiza, ninajivunia kuwa katika hii kazi na
ninauzoefu mkubwa na nimekuwa na uwezo wa kusimulia hadithi na kuwa sehemu ya
hadithi ambazo zinamaana na nimefanya mambo for fun, lakini...”, aliongeza ila
hakumalizia sentensi yake na kutabasamu.
‘The Salt’ actress alielezea mipango
yake kabla hajang’atuka katika tasnia hii ya uigizaji, “nitafanya movie kadhaa
na nina bahati nzuri sana kuwa na kazi hii, ni taaluma yenye bahati ukiwa sehemu
yake na ninaifurahia, lakini kama ntatoka kesho nitakuwa na furaha sana kuwa
nyumbani na watoto wangu. Naamka asubuhi kama mama na ninaangalia habari kama
mtu mwingine yeyote na naangalia nini kinatokea na nataka kuwa sehemu ya dunia
katika njia chanya.” Alimaliza Angelina Jolie
Post a Comment