Picha
mbalimbali zilizopigwa kutoka ofisi za walimu (staff room) zikionesha meza ya
kuchezea table tennis ikiwa ndani ya ofisi hiyo ya shule ya sekondari Bungu
Korogwe Vijijini.
Mkuu wa
Shule ya Sekondari Bungu, Dismas Kimweli (kushoto) akifanya mahojiano na Mhariri
wa Thehabari.com, Joachim Mushi alipotembelea baadhi ya Shule za msingi na
sekondari Halmashauri ya Korogwe juzi
---
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Bungu
iliyopo Korogwe Vijijini wamelalamikia kitendo cha baadhi ya walimu wao kucheza
mchezo wa table tennis ofisini (staff room) tendo ambalo limekuwa likifanyika
hata wakati wa kazi/vipindi vya masomo. Malalamiko hayo yametolewa juzi ambapo
mwandishi wa Thehabari.com alitembelea shule hiyo kuangalia changamoto
mbalimbali za elimu eneo la Korogwe Vijijini.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa
majina yao kiusalama na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wanafunzi hao
walisema wapo walimu ambao wamekuwa wakicheza mchezo huo hata wanapokuwa na
vipindi jambo ambalo huwakatisha tamaa wanafunzi. "Wapo baadhi ya walimu
wamekuwa wakijisahau na kucheza table tennis hata kama ni muda wa vipindi...na
endapo akiwaanacheza na kiongozi wa darasa asimfuate kumkumbusha kipindi anaweza
asije kabisa," alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Mwandishi wa habari hizi alifika shuleni
hapo na kuingia hadi ofisi ya walimu (staff room) na kushuhudia meza ya table
tennis ikiwa imefungwa katikati ya ofisi hiyo tena ikipewa nafasi kubwa zaidi ya
vifaa vingine vya kikazi vya walimu katika ofisi
hiyo.
Hata
hivyo mwandishi wa habari hizi alipozungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari
Bungu,Dismas Kimweli kutaka kujua sababu ya shule hiyo kuweka uwanja wa table
tennis ofisini hapo mwalimu huyo alisema wameufunga kwa muda kutokana na kukosa
eneo la kuuweka, lakini wanafanya jitihada za kuutoa uwanja
huo.
"Ni
kweli eneo hili kufungwa uwanja kama huo si sahihi...hili nalielewa lakini
tuliufunga kwa muda tu na hivi sasa tunajiandaa kuuamisha," alisema Kimweli.
Akifafanua zaidi alisema kutofundishwa kwa baadhi ya vipindi kwa wanafunzi
hakutokani na michezo ya table tennis shuleni bali uchache wa idadi ya walimu
shuleni hapo. Alisema kutokana na uchache huo wa walimu baadhi ya mwalimu huwa
na vipindi karibia 70 kwa wiki jambo ambalo huwazidi baadhi yao hivyo kujikuta
wakitupiwa lawama.
Shule
ya Sekondari Bungu iliyoanzishwa mwaka 1989 yenye jumla ya wanafunzi 640 ina
walimu 12 tu huku kati ya idadi hiyo walimu watatu kwa wako masomoni.
*Imeandaliwa na Kuletwa hapa na
Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na
HakiElimu
Post a Comment