| Sehemu ya ukuta uliobomoka |
Sehemu ya ukuta iliyobomoko na kusababishaa kifo cha mwanafunzi
mmoja
| Wasamaria wema wakijaribu kumwokoa kijana aliyeangukiwa na ukuta kwa kufukua kifusi kwa mikono |
Mwanafunzi wa kidato
cha pili katika shule ya sekondari Kwakilosa katika Manispaa ya Iringa
Daniel Yona (15) amefariki dunia baada ya kuaungukiwa na ukuta wa uwanja wa
Samora wakati akijaribu kupita mlango wa panya ili kwenda kushuhudia tamasha
hilo la Mtikisiko 2012.
Tukio hilo lilitokea
usiku wa kuamkia Desemba 2 mwaka huu wakati wapenda burudani katika mkoa wa
Iringa walipofika katika uwanja huo kushuhudia onyesho kubwa la Mtikisiko 2012
ambalo lilikuwa limepambwa na wasanii mbali mbali wakiongozwa na mkongwe Juma
Nature na Profesa J.
Wakielezea kilichomkuta
mwanafunzi huyo baada ya mashuhuda walisema kuwa mwanafunzi huyo na wenzake
waliacha kupita katika mlango wa kawaida kwa kulipia kiingilio halali
kilichowekwa na badala yake aliamua kupita gizani na kupanda ukuta huo wa
uwanja wa Samora ili kuweza kuingia ndani ya uwanja huo kuona tamasha la
Mtikisiko.
Hata hivyo mmoja kati
ya mashuhuda ambae hakupenda kutajwa jina lake hapa alisema kuwa kabla ya
mwanafunzi huyo kupanda ukuta huo kuna vijana kama 20 ambao walifanikiwa
kupita eneo hilo bila kulipa kiingilio na baada ya kufanikiwa kupita
walianza kupigiana simu huku baadhi ya vijana wa kitanzini wakiwatoza
vijana hao wanaoruka ukuta kiingilia cha shilingi 1000 hadi shilingi 500
.
"Ujue hapa vijana wa
kihuni kutoka Kitanzini walikuwa wamejipanga hapa na kufanya ufisadi wa
kuwatoza watu kiingilio bila wahusika wa Tamasha hilo kujua kinachoendelea
.....hivyo hata huyo mwanafunzi alikuwa ni mmoja kati ya wavamizi wa Tamasha
hilo kwa kupita njia ya panya ili kuingia ndani ya uwanja
huo"
Pia alisema ukuta huo
ulionyesha kuzidiwa nguvu kutokana na ubovu wa ukuta wenyewe kuwa ni mbovu
na ulikuwa umeungwa kienyeji katika eneo hilo .
Aidha alisema baada
ya vijana zaidi ya watano kupanda eneo hilo la ukuta ambalo lipo upande wa
kushoto mwa uwanja huo wa uwanja ukuta huo ulionyesha kuyumba na kupelekea
vijana wengine kuruka na kumwacha mwanafunzi huyo ambae tayari alikuwa
ameingiza mguu mmoja ndani ya uwanja na mguu wa pili ulikuwa
nje.
Alisema baada ya ukuta
huo kuanguka na kumfunika walifanikiwa kumwokoa akiwa hai na kumkimbiza
Hospitali ya mkoa wa Iringa ambako asubuhi ya siku ya pili ya Desemba 2 majira
ya saa 5 asubuhi alifariki dunia.
Hata hivyo askari
polisi waliokuwepo eneo hilo la tukio walimthibitishia mwandishi wa
mtandao huu kuwa ni kweli kijana huyo amefariki dunia japo wao si wasemaji
wa jeshi la polisi na kudai kuwa chanzo ni kijana huyo mwenyewe kutaka kupita
mlango wa panya na kuacha kupita mlangoni ambako watu wote walikuwa
wakipita bila kupata matatizo yoyote.
Hata hivyo uchunguzi wa
mtandao huu unaonyesha kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kimesababishwa na
mwanafunzi mwenyewe kutokana na kutaka kupita njia ya panya na kuacha mlango
kwani iwapo angetumia njia sahihi kuingia uwanjani yawezekana kifo kisingeweza
kutokea .
Source: Francis Godwin
Blog


Post a Comment