Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWANAHARAKATI WA HAKI ZA BIADAMU AKUTWA AMEKUFA GUESTI


Marehemu Eustace Nyaruganda
WANAHARAKATI wa waangaliza wa haki za binadamu kutoka nchi mbali mbali za Afrika Mashariki ambao wanaendelea na mafunzo ya uangalizi wa haki za binadamu jijini Daresalaam wameeleza kusikitishwa na taarifa za kifo cha mwanaharakati mwenzao haki za binadamu wa mkoa wa Mara Eustace Nyaruganda 45 aliyekutwa amekufa katika nyumba moja ya kulala wageni(Guest) mjini hapo.
Mbali ya kusikitishwa na mauwaji ya mwanaharakati mwezao huyo pia wameeleza kusikitishwa na kitendo cha kinyama alichotendewa mwandishi wa habari wa magazeti ya Free Media Shaban Matutu aliyepigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni askari polisi matukio waliyodai kuwa ni kinyume na haki za binadamu .
Wakizungumza leo katika mahojiano maalum na kipindi cha gali la matangazo la Radio Nuru Fm ya mkoani Iringa kutoka Hotel ya White Sands Kunduji jijini hapa wanaharakati hao akiwemo mwanaharakati aliyekuwa akifanya kazi na marehemu huyo mkoani Mara Angela Benedict na afisa shughuli wa shirika la ABC Foundation,Andreas Migiro walisema kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa juu ya taarifa za msiba wa mkurugenzi wake aliyekuwa amekufa asubuhi ya leo ikiwa ni baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku kadhaa .
Wakati Angela akidai kuwa taarifa ya kifo hicho imemshitua zaidi na kuomba uchunguzi wa kina wa kifo cha mwenzao huyo kutolewa bado kwa upande wake Migiro alisema kuwa alipewa taarifa kuwa mkurugenzi wao alikutwajana asubuhi akiwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Savana iliyoko katika mtaa wabenki mjini Bunda.
Akizungumzia kifo hicho cha mwanaharakati huyo,mratibu wa mtandao wa kutetea watetezi wa haki za binadamu nchini,Tanzania Human Right Defenders Coalitions, Onesmo ole Ngulumwa amesema kuwa mtandao umepokea kwa masikitiko makubwa sana juu ya kifo hicho na kwamba ni pigo kwa watetezi wa haki za binadamu kwani alimfahamu kwa karibu sana marehemu na kuwa kituo chake kitatoa taarifa kamili juu ya kifo hicho mapema leo .
Mratibu huyo alisema kuwa anatarajia leo kuongea na vyombo vya habari juu ya tukio la kifo hicho cha mwanaharakati ambapo pia amewaomba ndugu na jamaa wa karibu na marehemu ikiwa ni pamoja na jeshi la polisi kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ili mwili wake uweze kufanyiwa uchunguzi wa kina na dakitari kabla haujazikwa.
Hata hivyo baadhi ya wanaharakati wanaohudhilia mafunzo hayo wameonyesha kusikitishwa sana na mazingira ya kifo hicho ambapo wamesema kuwa hivi sasa maisha ya wanaharakati yako hatalini hivyo ni lazima waishi kwa tahadhali sana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalum Mwakyoma alipopigiwa simu alisema hana taarifa na tukio hilo na akasema apigiwe simu mkuu wa polisi wa wilaya hiyo ambapo yeye pia alisema yuko safari na kuelekeza kwa mkuu wa upelelezi wa wilaya ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na upelelezi zaidi.
Wakati huo huo mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania Absalom Kibanda akieleza kusikitishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea kufanywa na jeshi la polisi nchini na kuwa itafika wakati wanahabari nchini watahofia kufanya kazi na jeshi la polisi kutokana na vitendo hivyo vinavyoendelea kufanyiaka na kuona kama polisi ni maja ya maeneo ya hatari kwa wanahabari nchini .
Kibanda alidai kuwa anashindwa kujua sababu ya jeshi la polisi kumpiga risasi mwandishi wa gazeti la Tanzania daima Bw Matutu akiwa nyumbani kwake na kudai kuwa tukio hilo limefanyika kwa bahati mbaya na kuwa wao walikuwa wakimsaka mtuhumiwa wao wa kike na badala yake kumpiga mwanahabari huyo.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top