Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia saidi kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa India Dr. Inder Kumar Gujrat hapo ubalozi ndogo wa India uliopo Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif akimfariji Kaimu Balozi mdogo wa India aliyepo hapa Zanzibar Bwana D.J.M Rao pamoja na Ofisa wake mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha waziri Mkuu wa Zamani wa India Dr. Inder Kumar Gujrat.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ni miongoni mwa Viongozi wa Serikali,Mashirika na Taasisi mbali mbali za Kimataifa walioshiriki kuweka saini kitabu cha maombolezi kufutia kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani wa India Dr. Inder Kumar Gujral.
Dr. Inder Gujral alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika Hospitali moja ya kiraia Nchini india ambako alikuwa amelazwa tokea tarehe 19 Novemba mwaka huu baada ya figo zake kushindwa kufanya kazi.
Akipokewa na Kaimu balozi mdogo wa India aliyeko Zanzibar Bwana D.J Rao Balozi Seif alitia saini katika Ofisi ya Ubalozi huo iliyopo Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Dr. Gujrat aliyefikia umri wa miaka 92 alishika madaraka ya kuwa Waziri Mkuu wa 12 wa India kuanzia tarehe 21 Aprili mwaka 1997.
Katika uhai wake akiwa mtumishi wa serikali aliwahi kushika nafasi za uwaziri katika wizara tofauti, Balozi wa India Nchini Urusi pamoja na mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Nchi hiyo.
Katika Nyanja za Kimataifa Dr. Gujrat aliwahi kuwa mwenyekiti wa baraza la ushirikiano la Kusini mwa Asia, Mjumbe katika shirika la Unesco pamoja na mwakilishi wa umoja wa Mataifa katika kutatua baadhi ya mizozo Barani Afrika.
Kwenye harakati za Kisiasa na Uhuru Dr. Gujrat akiwa na umri wa miaka 11 alishiriki katika harakati za kudai uhuru wa Taifa hilo kwenye miaka 1931 hali iliyosababisha yeye na wenzake kuwekwa ndani na baadaye kufungwa jela mwaka 1942.
Katika uhai wake waziri Mkuu huyo wa zamani wa India Dr. Gujrat alikuwa akipenda kuandika vitabu mbali mbali pamoja na utangazaji kwenye hadhara za Kitaifa na Kimataifa.