Mkurugenzi wa Tahmini ya
Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo akitoa taarifa fupi
kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ambapo amesema
Wizara imetoa agizo la kufanya ziara katika Viwanda vilivyopo eneo la Mikocheni
na fukwe za hoteli zilizoko katika bahari ya Hindi maeneo ya Manispaa ya
Kinondoni kujionea changamoto za uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo ambayo
huleta athari kwa jamii kwa ujumla. Katikati ni Mkuu wa Msafara Naibu Waziri wa
Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na kulia ni
Mkemia Mkuu wa Mazingira katika Ofisi hiyo Bi. Rogathe
Kisanga.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya
kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga kutoka NEMC
akitoa maelezo kwa Naibu Waziri ambapo amesema NEMC imetoa agizo kwa wamiliki wa
Viwanda kuhakikisha wanafunga mitambo maalum yakusafisha maji taka yatokanayo na
bidhaa wanazozitengeneza hasa zinazotumia rangi kabla ya kuyamwaga katika mifumo
ya maji machafu ili kupunguza athari za uharibu wa
mazingira.
Naibu Waziri wa Nchi kwenye
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akizngumza na waandishi
wa habari kabla ya kuanza ziara ya kukagua Viwanda na Mahoteli yaliyopo maeneo
ya fukwe za bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam ambapo amewataka Watanzania
kuzijua na kuzifwata sheria za Mazingira ikiwemo sheria ya mwaka 2004 namba 20
inayowataka watu kutunza mazingira
yanayowazunguka.
Mwanasheria wa NEMC Bw.
Mwanchane Heche akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri kuhusiana na hatua zinazopaswa
kuchukuliwa kisheria kwa watu wanaochafua mazingira wakiwemo wanaomwaga maji
machafu yenye kemikali zinazoharibu Mazingira kutoka viwandani wakati wa ziara
ya kukagua Mto Mlalakuwa uliopo maeneo ya Kawe jijini Dar es
Salaam.
Huu ndio Mto Mlalakuwa Kawe
Darajani unavyoonekana ambapo maji yake yanaonyesha kuchafuliwa na maji taka
yatokayo viwandani.
Mkurugenzi wa Tahmini ya
Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo akifafanua jambo kwa
Mh. Charles Kitwanga wakati wa ziara hiyo sambamba na jopo la waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali.
Eneo la Mto Mbezi lenye
mgogoro kufuatia kuzuia mtiririko wa maji ya Mto huo ambalo limenunuliwa na mtu
Binafsi anayefahamika kwa jina la Robert Mgishwagwe ambaye kila anapofuatwa na
vyombo husika kumtaafiru kwamba eneo hilo haliruhusiwi kujengwa amekuwa akikaidi
na kudai kwamba yeye ni mfanyakazi wa Usalam wa Taifa. Kitendo cha kuweka Kifusi
na kukisawazisha katika njia ya maji ya mto Mbezi na kimesababisha Daraja
lililopo kando ya eneo hilo kuvunjika kila mara na kusababisha usumbufu kwa
wananchi.
Post a Comment