NaibuWaziriwa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki
akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Tume ya Mabadiliko ya Katiba
katikauzinduzi wa maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani leo jumatano
Disemba 5, 2012 zinazoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mjumbewa Sekretarieti yaTume hiyo, Bw. Andrew
Eriyo.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Bw. Andrew Eriyo akitoa ufafanuzi wa kazi na majukumu mbalimbali yaTume hiyo kwa
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) wakati
alipotembelea banda la Tume hiyo leo (Jumatano Disemba 5, 2012) katika
maadhimisho ya siku ya Hakiza Binadamu zinazoendelea katika viwanja vya Mnazi
Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Amour Kagya (kulia) akigawa nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na
machapisho mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo kwa wananchi waliotembelea banda
la Tume hiyo leo (JumatanoDisemba 5, 2012) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya
siku ya Haki za Binadamu Duniani zinazofanyika kitaifa katikaViwanja vya Mnazi
Mmoja Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA TUME YA
KATIBA)
on Thursday, December 6, 2012
Post a Comment