Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Sebastian Nandi akimuonyesha eneo la Bandari ya Kasanga, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki), leo asubuhi. Naibu Waziri wa Uchukuzi yuko Mkoani Rukwa kwa ziara ya kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki), akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), alipotembelea Bandari ya Kasanga Mkoani Sumbawanga leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki), akiangalia mzigo wa Saruji, uliohifadhiwa kwenye magodauni ya Mamlaka ya Bandari ya Kasanga, alipotembelea bandari hiyo leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba (aliyevaa suti ya kaki ),akiangalia maporomoko ya Kalambo yaliyoko Mkoani Rukwa leo asubuhi. Maporomoko hayo ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika, ya kwanza yakiwa yale ya Viktoria Falls yaliyoko Zimbabwe.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki), akibadilishana mawazo na Mtendaji wa kijiji cha Kapozwa Sumbawanga, Bw. Abeid Mwanakatwe (aliyevaa flana ya rangi ya Maziwa)mara baada ya kuangalia maporomoko ya Kalambo leo mchana.
Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi na Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege(TAA), Mhandisi George Sambali, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki),ya namna ambavyo Uwanja wa Ndege Mpya Unaotaka kujengwa katika eneo la Kisumba mkoani Sumbawanga utakavyokuwa leo mchana.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki),akifafanua jambo kwa uongozi wa kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga katika ofisi za kiwanja hicho leo Mchana.
Muonekano wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga. Kwa mwaka 2012 idadi ya abiria imefikia wastani wa 200 kwa Mwezi ikilinganishwa na miaka ilipita na matarajio kufikia mwishoni mwa mwaka 2012 idadi ya abiria itazidi na kufikia 1,000.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki),akisistiza jambo kwa uongozi wa Kiwanja Cha Ndege Cha Sumbawanga leo Mchana,alipotembelea kiwanja kujionea namna kinavyofanya kazi.Naibu Waziri ameuagiza uongozi wa kiwanja hicho pamoja na mambo mengine kuhakikisha wanaweka uzio maana Wananchi wanapita katikati ya uwanja huo kwa sababu ya kukosa Uzio.