Ndege yashirika la
hifadhi la taifa (TANAPA) yenye namba za usajili 5H-PZS aina ya C182 ikiwa
imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka
katika uwanja wa ndege wa mjini mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa
aliepata majeraha sehemu ya uso. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10:55 jioni
wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa
katavi. picha na walter mguluchuma
*****
na walter
mguluchuma,mpanda
Ndege ya hifadhi ya
taifa ya TANAPA imepata ajari ya kuanguka wilayani Mpanda mkoa wa
Katavi na rubani wa ndege hiyo kunusurika kifo baada ya kupata
majeruhi
Meneja wa uwanja wa
ndege wa Mpanda Mahamud Muhamed alisema ajari hiyo ilitokea jana majila
ya saa 10 na dakika 55 jioni katika kijiji cha Nsemlwa wilayani
hapo
ndege
hiyo iliyo anguka ilikuwa namba za usajiri 5H-- FZS aina ya C182 ndege
ndogo ya abiria mari ya hifadhi ya taifa ya TANAPA iliyo kuwa ikiendeshwa na
rubani Adamu Athumani Kajwaa yenye uwezo wa kuchukua
abiria wane
Muhamed alieleza
kuwa ndege hiyo ilikuwa imetoka katika uwanja wa ndege wa
mpanda ikielekea katika hifadhi ya wanyama pori ya Katavi wilayani
Mlele
Ajari hiyo ilitokea umbali
wa kilimeta moja na nusu kutoka uwanja wa ndege wa
Mpanda mara baada ya kuondoka katika uwanja huo ambapo imeharibika sana
sehemu ya bawa lake na upande wa injini.
Meneja wa uwanja huo
wa ndege alisema taarifa za awali zinaonyesha chanzo cha
ajari hiyo kilitokana na njini ya ndege hiyo kufeli wakati ikiwa
angani
Rubani wa ndege
hiyo alipata msaada wa wa kuokokewa
na wananchi waliokuwa wakifanya shughuli za kilimo kwenye mashamba yao
Mmoja wa walio shuhudi
tukio hilo Credo Mwanisenga alieleza kuwa wakati akiwa anafanya
shughuli zake za
kilimo ghafla aliona ndege iliyo kuwa angani ikizimika na kisha baada
ya muda mfupi ikaanguka jirani na mti wa
mwembe
Na mara walifika katika
eneo hilo kwa lengo la kutowa msaada hata hivyo iliwachukuwa muda kuanza
kutowa msaada kwa rubani huyo aliye kuwa ndani ya ndege peke
yake kutokana na eneo hilo kuwa na nyuki wengi ambao walianza kuwashambulia
waokoaji hao
Hata
hivyo waliewza kufanikiwa kumtoa rubani huyo huku akiwa amepata majeruhi
makubwa sehemu ya uso wake na maumivu sehemu ya kifua huku akiwa anakohoa
damu na aliewza kukimbizwa haraka katika hosptali ya wilaya ya mpanda baada
ya kupata msaada wa gari la meneja wa uwanja wa ndege aliye fika kwenye
eneo la tukio
Rubani wa ndege hiyo
aliweza kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya yam panda kwa kushonwa
nyuzi nane katika paji la uso wake na kasha aripewa ruhusa.
Post a Comment