Shabaan Matutu akionesha
sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha wakati polisi walipotumia
nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga risasi iliyompiga upande wa kushoto wa
kifua chake.
Mwandishi wa habari wa
Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari,
Shaaban Matutu akionesha jeraha lililotokana na kupigwa risasi na Polisi katika
tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo - baada ya polisi kuvamia nyumbani kwake
Tegeta jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumtafuta mtuhumiwa waliyekuwa
wakimsaka. Matutu kwa sasa amelazwa Hospitali ya Muhimbili katika Kitengo cha
Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.
Shabaan Matutu akionesha
sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha wakati polisi walipotumia
nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga risasi iliyompiga upande wa kushoto wa
kifua chake.
Daktari aliyekuwa zamu
katika Hospitali ya Mwananyamala akiangali picha ya X-Ray ya Matutu mara baada
ya kufikishwa katika hospitali hiyo na kufanyiwa kipimo hicho, kabla ya
kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu
zaidi.
Wafanyakazi wa Free Media,
Khadija Kalili kushoto na Maria Kayala (kulia) ambao walifika Hospitali ya
Mwananyamala baada ya kupata taarifa za tukio hilo.Picha Zote na Habari na Dande
Francis
Post a Comment