Waziri Mkuu
Mizengo akipalilia mahindi ili kumwonyesha Bi. Yusta Kipande namna ya kupandisha
udongo kwenye mche wa muhindi wakati wa palizi wakati akikagua shamba la Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Desemba 18, 2012 eneo la tenki fupi kata ya Nsimbo, wilayani
Mlele, Katavi. Bi. Kipande ni
mfanyakazi katika shamba hilo.
Waziri Mkuu Mizengo akipokea maelezo ya shamba
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Rajab Rutengwe (wa pili kulia) wakati
alipoenda kukagua shamba la Mkuu huyo wa Mkoa Desemba 18, 2012 eneo la tenki
fupi kata ya Nsimbo, wilayani Mlele, Katavi. Kulia ni Bi. Yusta Kipande na
(kushoto) ni Bi. Grace Donald wanaofanya kazi kwenye shamba hilo
.
Waziri Mkuu Mizengo
akipokea maelezo ya shamba
kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Injinia Emmanuel Kalobelo
(aliyenyoosha mkono) wakati alipoenda kukagua shamba lake Desemba 18, 2012 eneo
la tenki fupi kata ya Nsimbo, wilayani Mlele, Katavi. (Picha na Irene Bwire wa
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Post a Comment