Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni ACP Charles Kenyela (pichani) akitoa taarifa ya msako wa kupambana na
wahalifu kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kusema jeshi la polisi mkoa wa
Kinondoni limefanikiwa kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali na vielelezo
kadhaa.
Amesema wamewakamata
watuhumiwa watano wanajihusisha na biashara ya kujiuza kimwili na utali au wizi
kwa wateja wao ambapo walikutwa na vidonge vya aina mbalimbali pamoja na unga
uliosagwa vyote vikidhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya ambayo hutumia kuwawekea
wateja wao.
Katika msako huo
wamekamatwa watuhumiwa 17 wanaojihusisha na biashara ya bhangi, gongo, kamari na
kubugudhi abiria huku vielelezo vilivyokamatwa ni bhangi kilo moja na nusu na
puli 300, gongo lita 35 na kete 20 za madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa ni
Heroen.
Msako huo ndani ya saa 24
umemkamata mtu mmoja aitwaye Haji Juma mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Kawe
Ukwamani akiwa na silaha Bastola aina ya Browning No. A 080416 iliyotengenezwa
Czechlovakia.
Aidha Kamanda Kenyela
amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linaendelea na Operesheni zake kwa
njia ya misako na doria ili kuwabaini madereva wa magari na pikipiki ambao
wanakiuka Sheria za Usalama Barabarani na kusababisha ajali
mbalimbali.
Kati ya kipindi cha mwezi
Novemba hadi Desemba jumla ya magari na pikipiki 2,339 yalikamatwa kwa makosa
mbalimbali ya usalama barabarani ambapo madereva walitozwa faini za hapo kwa
papo (Notification) zilizofikia Shilingi 81,390,000/= na magari mengine 20
yalitozwa faini na SUMATRA ya jumla zaidi ya Shilingi
5,000,000/=.
Post a Comment