Waziri wa Nishati na Madini
Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha
Wafanyabiashara ya Madini (TAMIDA), Bw. S. Sammy Mollel walipokutana katika
makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili masuala mbalimbali
yanayohusiana na biashara ya madini nchini ikiwa ni pamoja na ufungaji na
usafirishaji wa vifurushi na mizigo ya madini, ongezeko la kodi ya thamani ya
asilimia 18 ya madini, bei elekezi ya uuzaji wa madini inayotolewa na TANSORT,
ada za leseni za wafanyabiashara na uombaji wa kibali maalumu kwa watalii
wanaonunua madini ya vito kwenye maduka ya vito.
Waziri wa Nishati na Madini
Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizokuwa
zikijadiliwa na Wafanyabiashara wa Madini nchini ambapo aliunda kamati maalumu
ambayo itahusika na upangaji wa bei elekezi ya madini. Kamati hiyo itahusisha
wajumbe mbalimbali kutoka wizarani, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na
Wawakilishi kutoka Chama cha Wafanyabishara ya Madini nchini (TAMIDA). Kamati
hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthamini wa Almasi na Vito
Tanzania. (TANSORT)




Post a Comment