
Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar
zinaanza rasmi hapo Januari, 4 mwezi ujao kwa Wilaya za Unguja na Pemba kufanya
usafi wa Mazingira katika maeneo yao.
Kwa mujibu wa Ratiba iliotolewa na
Kamati ya sherehe hizo imeonesha kuwa miradi 62 itazinduliwa na mengine kuwekwa
jiwe la msingi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Ratiba hiyo
imeonesha kuwa tarehe 5mwezi ujao asubuhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein atafunguwa Jengo la Chuo cha Utawala
wa Umma ,huko Tunguu Wilaya ya kati Unguja Mkoa wa Kusini Unguja.
Jioni
Dkt Shein atafunguwa mradi wa E -Government Mazizini Wilaya Magharibi
Unguja.
Tarehe hiyo hiyo 5 asubuhi Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad huko Kisiwani Pemba atafunguwa Skuli mpya ya Sekondari
ya Wawi iliopo Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba na jioni atafunguwa
Maabara katika Hospitali ya Cottage ya Micheweni Mkoa
wa Kaskazini
Pemba.
Nae Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif
Ali Idd jioni huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi Unguja atafunguwa Bweni la
Wanafunzi wa Kilimo.
Mnamo tarehe 6 asubuhi huko Maruhubi Wilaya ya Mjini
Unguja Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dtk Ali Mohamed
Shein atafunguwa Bohari Kuu ya Dawa ambapo jioni siku hiyo Rais Mstaafu Dkt
Amani Abeid Karume atafunguwa skuli mpya ya Sekondari huko Muwanda Wilaya ya
Kaskazini B Mkoa wa Kaskani Unguja.
Mbali na shughuli hizo pia Dkt Shein
tarehe 7 atafunguwa Skuli mpya ya Sekondari ya Uzini ilipo Wilaya ya Kati Unguja
Mkoa wa Kusini Unguja ambapo jioni huko Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal
atafunguwa Hoteli ya Nyota tano.
Kisiwani Pemba siku hiyo jioni Makamo wa
Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Makangale, Wilaya ya Micheweni
atafunguwa Hoteli ya Ndani ya Maji,"MANTA REEF RESORT"na asubuhi Wilaya ya Mkoa
Michenzani Chokocho atafunguwa Mradi wa Maji Safi na Salama.
Asubuhi ya
tarehe 8 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed
Ali Shein hapo Raha Leo Wilaya ya Mjini Unguja atafanya ufunguzi wa Mradi wa
kuhama kutoka Teknologia ya Analojia kwenda Dijitali na ufunguzi wa Studio ya
kurikodi sanaa na Muziki.
Asubuhi hiyo hiyo huko Micheweni Pemba Makamo
wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd atafunguwa kituo cha Afya kiliopo
Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba ambapo asubuhi hiyo hiyo katika Wilaya ya
Kaskazini A, Unguja Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi atafunguwa Skuli mpya
ya
Sekondari ya Mapinduzi iliopo Chaani Wilaya ya Kaskazini A.
Jioni
katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja Dkt Shein atafunguwa Barabara ya Mfenesini
hadi Bumbwini ambapo tarehe 9 Wilaya ya Kaskazini A Unguja Makamo wa kwanza wa
Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad atafunguwa Skuli ya Msingi iliopo mbuyu
Mtende
Tarehe 10 jioni kutakuwapo na ufunguzi wa Mradi wa "One World
Football for Africa ambapo Rais wa Zanzibar Dkt Shein atakuwa Mgeni rasmi kwenye
Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar na asubuhi Balozi Seif Ali Idd huko Dole Wilaya
ya Magharibi Unguja atafunguwa Skuli Mpya ya Sekondari ya Mikindani iliopo
Dole.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd tarehe 11
asubuhi atafunguwa Majengo Mapya ya Nyumba za Wazee Sebleni zilopo Wilaya ya
Mjini Unguja na jioni huko Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete atafungua Skuli mpya ya
Sekondari ya Mlimani.
Usiku siku hiyo katika Wilaya ya Mjini Unguja
kutakuwa na maonesho ya Ngoma za Utamaduni na Muziki katika Mesi ya Polisi
Ziwani na pia kupigwa Mizinga, Kurushwa Fash Fash na Meli ziliopo Bandarini na
Gari ziliopo Barabarani zitapiga Honi na Ving'ora.
Tarehe 12 ndio
kilele cha Sherehe ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt Ali Mohamed Shein atakaguwa Gwaride Rasmi la Vikosi vya Ulinzi na Usalama na
Vikosi vya Serikali Mapinduzi Zanzibar pamoja na Maandamano ya Wananchi wa Mikoa
mitano ya Zanzibar na baadae kulihotubia Taifa huko katika Uwanja wa
Amani,
Mbali na Shughuli hizo za uzinduzi wa Miradi mbali mbali
zitakazofanywa na Viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Tanzania,
pia Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano
watazinduwa na kufunguwa Miradi mbali mbali ukiwamo ule wa
Ufunguzi wa Mnara
wa Redio wa Masafa ya Kati ambapo Waziri wa Mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Prof,Makame Mbarawa atafunguwa na pia
kuwekwa jiwe la msingi Skuli ya Moga Wilaya ya Kaskazini A Unguja ambapo Naibu
Waziri wa
Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bihindi Hamad Khamis
ataifanya kazi hiyo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
on Tuesday, December 25, 2012
Post a Comment