Sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya chama tawala cha RPF zinafanyika katika uwanja taifa wa Amahoro mjini Kigali, ambapoa rais Paul Kagame wa Rwanda aliye pia Mwenyekiti wa taifa wa Chama hicho atalihutubia kuhutubia taifa.
Sherehe hizo pia zinahudhuriwa na rais wa Uganda Yoweri Museveni aliyekisaidia sana Chama hicho kuwepo madarakani.
Chama cha RPF ‘Inkotanyi’ kiliasisiwa nchini Uganda mwaka 1987 na wakimbizi wa kitutsi wengi waliokuwa katika kambi za wakimbizi nchini humo, madhumini makubwa yakiwa ni kurejesha wakimbizi waliokimbia Rwanda mnamo mwaka 1959 kufuatia machafuko ya kikabila yaliyotokana na harakati za kutafuta uhuru, ambapo wakereketwa wa kihutu wakisaidiwa na wabelgiji walipindua utawala wa kifalme.
Mwaka 1990 majeshi ya RPF yakitokea nchini Uganda yalianzisha vita vya msituni dhidi ya utawala wa hayati Juvenal Habyarimana uliokuwa ukituhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji ya kimbari na kuung’oa madarakani utawala huo mwaka 1994.
Sasa imetimia miaka 18 tangu chama hicho kushika hatamu huku RPF ikijivunia kuiweka Rwanda mahali pazuri kiasi cha kusifiwa na mataifa ya kigeni, kwa uchumi kuimarisha miundo mbinu, elimu na afya lakini zaidi ni kuweza kuwaweka pamoja jamii ya Wanyaruanda na kuondokana na suala la ukabila.
Post a Comment