KWA UFUPI
Kikosi hicho kisichofungamana na upande wowote
kinatazamiwa kutumwa Mashariki kwa Congo wakati wowote, baada ya kukamilika kile
kilichoelezwa hatua za awali za utendaji ambazo zinaratibiwa na asasi ya ulinzi
na amani (troika), ambayo inasimamiwa na Tanzania, Namibia na Afrika
Kusini.
Baadhi ya Viongozi wa nchi za SADC
JUMUIYA ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc), imepanga
kutumia dola 100 milioni za Marekani kukabiliana na kundi la waasi wa M23
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kiwango hicho ni sawa na
Sh160 bilioni (dola moja kwa Sh1,600), kinatazamiwa kutumika kugharimia
operesheni za vikosi vya kulinda amani ya jumuiya hiyo, ambavyo vinakusudiwa
kutumwa eneo hilo lenye uasi.
Viongozi wa Sadc waliokutana Dar es Salaam kwa kikao
cha dharura kujadilia hali ya amani nchini DRC, walikubaliana kugharimia kikosi
hicho na wamewaonya waasi hao kuondoka maeneo wanayokalia.
Kikosi hicho kisichofungamana na upande wowote
kinatazamiwa kutumwa Mashariki kwa Congo wakati wowote, baada ya kukamilika kile
kilichoelezwa hatua za awali za utendaji ambazo zinaratibiwa na asasi ya ulinzi
na amani (troika), ambayo inasimamiwa na Tanzania, Namibia na Afrika
Kusini.
Tanzania na Afrika Kusini zimeahidi kuchangia sehemu
kubwa ya gharama kufanikisha operesheni za kikosi hicho, uamuzi ambao
umepongezwa na nchi wanachama wa Sadc. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa vikosi
vya Sadc kutumwa nchi wanachama kuzima uasi.
WAKIMBIZI WA DRC.
Akitangaza maazimio ya kikao hicho,
Rais Jakaya Kikwete alisema nchi kumi eneo la Maziwa makuu zimekubaliana kuunda
jeshi hilo, litakalokuwa na askari 4,000 kukabiliana na ghasia na vita ya mara
kwa mara Mashariki mwa Congo.
“Kimsingi tumekubaliana kuunda jeshi na jukumu letu la
kwanza litakuwa kwenda kusimamia hali ya amani huko Congo, pande zote
zimekubaliana kuchangisha fedha kuliwezesha jeshi hilo kuendesha operesheni
zake kwa ufanisi zaidi,” alisema Rais Kikwete.
Alisema kikao cha viongozi wa Sadc wamelaani vikali
hujuma zinazoendelezwa na waasi wa M23, ambao hivi karibuni walifaulu kuteka
mji wa Goma na maeneo mengine ya jirani.
Post a Comment