Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi akiwa
Mwenyekiti wa wake za viongozi, Germina Lukuvi mara baada ya timu ya Taifa ya
Netiboli (Taifa Queens) iliporejea nchini na Kombe la Michiuano ya Kimataifa
iliyofanyika nchini Singapore.
Baadhi ya wachezaji wa timu
ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’ wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo wakitokea Singapore
walikokuwa wakishiriki michuano ya Kimataifa na kutwaa Kombe la michuano
hiyo.
Mlezi wa Chaneta kupitia Kamati ya Olimpiki
Tanzania (TOC), Ain Sharif akikabidhi kitita cha sh. 500,000 ikiwa ni kama
zawadi kwa timu hiyo baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa
yaliyofanyika Singapore na Taifa Queens kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Wachezaji na viongozi wa timu
ya Taifa ya Netiboli (Taifa Quees) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao
baada ya kuwasili leo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
wakitokea nchini Singapore.
Na Mwandishi
Wetu
TIMU ya taifa ya Netiboli ya
Tanzania ‘Taifa Queens’ imerejea kwa kishindo leo baada ya kushiriki na kutwaa
Kombe la michuano ya Kimataifa iliyokuwa ikifanyikia Singapore barani
Asia.
Taifa Queens ilitwaaa ubingwa
huo baada ya kuingia fainali ikiwa na pointi 10 ikicheza na timu ya Malasia
iliyokuwa na pointi 4 ambapo ilifanikiwa kuifunga magoli 45-38.
Akizungumza baada ya kurejea,
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi alisema
maandalizi ni kitu kizuri sana, anaamini kocha aliwapa wachezaji mbinu za
kutosha hadi kupelekea ubingwa huo.
“Hii imetusaidia sana maana
kocha mwenyewe ni kijana hivyo anambinu za kisasa kitu kilichotusaidia wakati
tukiwa ugenini, hakuna kitu kizuri kama kupigiwa wimbo wa taifa lako ukiwa
ugenini huku wazungu ambao ni wenyeji wa mashindano hayo wakiwa penbeni,”
alisema Bayi.
Kwa upande wake Kocha wa
Taifa Queens, Mary Waya alisema mashindano yalikuwa ni magumu anawapongeza
wachezaji wake kwa ushindi huo ambao umemuweka pazuri yeye pamoja na Watanzania
wote kwa ujumla.
“Kila kitu unatakiwa
umtangulize mungu, akili, na nguvu ndio zinafuata naimani wachezaji wangu
walikuwa makini na kujua nini wamekifuata huko, akili ni kitu cha muhimu ukiwa
mchezoni hivyo mimi sina la kusema zaidi ni kumshukuru mungu kwa ushindi
tulioupata,” alisema Kocha huyo ambaye ni Mmalawi.
Kocha huyo alisema
amefurahishwa na ushindi huo na kwamba kwasasa anajipanga kuifua timu hiyo
kwaajili ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia.
Naye Nahodha wa timu hiyo,
Lilian Sadolin alisema anamshukuru mungu kwa ubingwa huo pia Watanzania
wanatakiwa kuendelea kuwapa sapoti katika mashindano
mbalimbali.
“Wakati tunaondoka
niliwaahidi Watanzania lazima turudi na ushindi, sisi ubingwa tushaapata kabla
hatujaenda kule tulienda kutimiza wajibu, naimani tuliwazidi mbinu unapokuwa
uwanjani unatakiwa kuwa na mbinu za ziada hivyo tunamshukuru mungu kwa ushindi
tulioupata,” alisema Lilian.
Mwisho.
Post a Comment