Waziri
wa fedha na uchumi Dkt Wiliam Mgimwa akifungua mafunzo ya wajasiriamali
yaliyoandaliwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Ritta
Kabati
Baadhi
ya wawakilishi wa vikundi wakisikiliza mafunzo ya ujasiriamali katika ukumbi wa
hallfare
Waziri wa Fedha Dr
William Mgimwa akimkabidhi Mbunge wa Viti maalum (CCM) Ritta Kabati kiasi cha
milioni 1kwa ajili ya kuchangia kwa vikundi vya ujasiriamali(picha na Denis
Mlowe)
WAZIRI wa fedha na
uchumi Dk Wiliam Mgimwa ametangaza vita kali kwa mafisadi wanaoficha fedha
katika mabenki ya nje ya nchi .
Mwandishi wa mtandao
huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Iringa Denis Mlowe anaripoti kuwa
,Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Dr William Mgimwa leo wakati akizungumza na
waandishi wa mkoani Iringa mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa
vikundi 29 vilivyoko mkoani hapa vinavyofadhiliwa na mbunge wa viti maalum
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Ritta Kabati
.
"Serikali
itawashughulikia watu wote wanaoweka fedha nje ya nchi kwa njia haramu ....
inafatilia kwa karibu sana wale walioweka fedha hizo nje ya kwa nchi kwa
kuwasiliana na nchi zinazosemekana mafisadi wanaweka fedha hizo na haina hofu na
kundi au mtu wanaosemekana wanaweka fedha katika mabenki ya nje ya
nchi"
Alisema kuwa dawa ya
watu hao wanaoficha fedha nje ya nchi ipo jikoni na kusema kuwa serikali
haitalala katika kuwashughulikia watu hao wa kuchukua hatua
zaidi.
Hatua hiyo ya waziri
wa fedha kutangaza uamuzi huo imekuja huku zikiwa zmepita siku chache
toka naibu katibu mkuu chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Zitto Kabwe
kutaka serikali kuwabana wale wote wanaoficha fedha nje ya nchi na kutaka
fedha hizo kurejeshwa nchini.
Awali akifungua mafunzo
hayo ya ujasiriamali katika ukumbi wa Orofea mjini Iringa Dk Mgimwa mbali ya
kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali
hao pia aliwataka wajasiriamali mkoani Iringa kutumia mafunzo hayo katika
kujiongezea kipato .
Kwa upande wake mbunge
Kabati alisema kuwa mafunzo hayo ni moja kati ya ahadi zake kwa wajasiriamali
mkoani Iringa na kuwa lengo ni kuendelea kutekeleza ahadi zake zaidi
.
Alisema kuwa mafunzo
hayo yanatolewa na taasisi ya ujasiriamali ya Decision Foundation ya kutoka
Dar es Salaam .
Hata hivyo Kabati
alisema kuwa kuwa serikali ya CCM imeendelea kuonyesha mfano katika
uwajibikaji kwa wananchi wake na kuwa lengo ni kuona wanaendelea kuwa na
imani ya CCM na serikali yake .
"Ndugu zangu wananchi
mbali ya mafunzo haya nimeendelea kuwa jirani na wananchi wangu wa jimbo la
Iringa mjini kwa kuwawezesha vijana na kuanzisha vikundi vya benki za
wananchi mitaani (VICOBA) pamoja na kuwasaidia watu wenye makundi mbali mbali na
sitachoka kufanya hivyo"
MWISHO
Waziri wa fedha na uchumi Dkt Wiliam Mgimwa akifungua mafunzo ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Ritta Kabati |
Baadhi ya wawakilishi wa vikundi wakisikiliza mafunzo ya ujasiriamali katika ukumbi wa hallfare |

Post a Comment