Msemaji
wa Simba Ezekiel Kamwaga.
26/12/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KHERI ya Krismas na Mwaka
mpya kwenu nyote.
Uongozi wa klabu ya Simba
leo unapenda kutoa taarifa ifuatayo kwenu.
- Mkutano wa Wanachama
uliopangwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu.
UONGOZI umepata taarifa
kuwa kuna kundi la wanalojiita wanachama wa Simba waliopanga kufanya mkutano wa
wanachama siku ya tarehe 30 Desemba mwaka huu (Jumapili hii) kwa lengo la
kujadili mambo ya klabu.
Mkutano huo, kwa mujibu wa
Katiba ya Simba ni batili. Ubatili huo unatokana na ukweli kwamba wale
walioutisha mkutano huo hawana Locus Standi (nguvu au mamlaka) ya kufanya
hivyo. Katiba ya Simba iko wazi kuwa mtu anayeitisha mkutano wa wanachama ni
MWENYEKITI wa klabu pekee na si vinginevyo.
Mkutano huo wa wanachama
haujaitishwa na Mwenyekiti wa klabu na hivyo hauna uhalali wowote wa
kisheria.
Uchunguzi uliofanywa na
klabu umebaini kwamba zaidi ya nusu ya walioitisha mkutano huo pia si wanachama
halali wa Simba. Wengine hawajawahi kulipa ada zao za uanachama katika kipindi
cha hadi miaka 10 iliyopita !
Matendo yanayofanywa na
kundi hili yanaashiria watu wanaotaka tu kuleta vurugu klabuni. Kundi hili
linafanya hivi wakati Rais Jakaya Kikwete ametoka kutoa kauli kuhusiana na namna
vurugu zinavyosababisha kushuka kwa michezo hapa nchini.
Kundi hili linaandaa vurugu
katika kipindi ambacho uongozi upo katika mikakati kabambe ya kuiboresha timu
ikiwamo kuipeleka nje ya nchi kufanya mazoezi, jambo ambalo halijawahi kufanyika
katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Linaandaa vurugu katika
kipindi ambacho Simba ndiyo bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania na ikiwa
imeongoza ligi katika msimu huu kuanzia mechi ya kwanza hadi ya 11 katika mechi
13 za kwanza.
Klabu inaomba wapenzi na
wanachama wake kukaa mbali na kundi hili la waleta vurugu. Huu ni wakati ambapo
tunatakiwa kuwa pamoja kwa vile klabu inatakiwa kutetea ubingwa wake na pia
kuliwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa mapema
mwakani.
Huu ni wakati wa wanachama,
wapenzi na uongozi kuwa kitu kimoja. Uongozi uko tayari kukosolewa wakati wowote
ule lakini haukubaliani na waleta vurugu.
Uongozi unapenda kusisitiza
lifuatalo, Mkutano wa Desemba 30 ni batili na wale wote wenye mapenzi mema na
klabu wanatakiwa kukaa mbali nao na kutojihusisha kwa chochote na wanaopanga
vurugu.
Imetolewa
na
Ezekiel
Kamwaga
Ofisa
Habari
Simba SC
Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga. |
26/12/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KHERI ya Krismas na Mwaka
mpya kwenu nyote.
Uongozi wa klabu ya Simba
leo unapenda kutoa taarifa ifuatayo kwenu.
- Mkutano wa Wanachama uliopangwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu.

Post a Comment