Kama unakumbuka kwenye consert ya Summer Jam mwaka huu ambayo huandaliwa na kituo maarufu cha radio cha Marekani HOT 97 kuna mtangazaji mmoja aitwae Rosenberg alipokua kwenye stage ya hiyo Fiesta yao a.k.a Summer Jam alimchana rapper Nicki Minaj kwa kusema aliacha kufanya hiphop na kuanza kufanya muziki wa pop kitu ambacho kitamuharibia mwelekeo wake wa muziki.
Sasa hivi Nicki Minaj ametoa album ya Pink Friday the re-up, hii ni ile ile album kama ya mwanzo ila kwenye hii mpya kaongeza track 6 ambazo nyingi ni hiphop zaidi ya pop.
Kwenye wiki ya kwanza imeuza kopi elfu 36 tu kitu ambacho ni kibaya sana kwa staa kama yeye, baada ya Msanii mkubwa kama Nicki kuporomoka hivyo kwenye mauzo, watangazaji wengine wa Hot 97 wakaongea kwenye show kwamba Rosenberg alipomchana Nicki ni kama alitabiri na alikua sahihi
Baada ya hao watangazaji kuongea hivyo, mkuu wa vipindi wa Hot 97 anasema alipokea simu kutoka kwa Nicki Minaj ambae alizungumza maneno yote makali ambayo wanawake huwa wanatumia kuwatukana wanaume, akamuita rafiki wa uongo na tapeli na kusema ameambiwa na watu huyu mshkaji sio mtu mzuri.
Ebro ambae ndio mkuu wa vipindi akamjibu Nicki akisema “mimi nilikua najaribu kukujenga maana najua hiphop ina ushindani na usipobaki kwenye ramani ya hiphop usipozungumziwa kwenye hiphop utasahaulika, nakupenda sana Nicki na hata kikiharibika au ukianguka nitakuinua na kukurekebisha ulipokosea, ndio hapo Nicki Minaj akanitamkia kwamba kwanza msicheze tena nyimbo zangu kwenye radio yenu”

Post a Comment