Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) akitoa taarifa ya serikali kwa vyombo vya habari kuhusu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2012, ambapo pamoja na kuzungumzia usajili wa watahiniwa, Matokeo ya mtihani, uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza 2013 na udanganyifu katika mitihani, pia amewaasa wanafunzi wote waliochaguliwa kutumia fursa hiyo vizuri kwa kujifunza.
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 560,706 kati ya 865,534 waliofanya mtihani wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali, ambapo idadi hiyo ni sawa na asilimia 64.78 ya wanafunzi waliofanya mtihani.
Aidha kati ya wanafunzi waliochaguliwa wasichana ni 281,460 sawa na asilimia 50.20 na wavulana ni 279,246 sawa na asilimia 49.80.
Pia takwimu zinaonyesha waliofutiwa matokeo kutokana na vitendo vya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2012 imepungua sana, kwani ni watahiniwa 293 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliofutiwa matokeo mwaka 2011.
Post a Comment