Timu ya
soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, (Taswa FC) ni miongoni mwa timu
nane zitakazoshiriki katika bonanza maalum la kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa
Tanzania (Uhuru Dar Corporate Bonanza) lililopangwa kufanyika Desemba 9 kwenye
uwanja wa Gymkana.
Mwenyekiti
wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wamepokea mwaliko kutoka kwa Mkurugenzi
wa Kampuni ya Vannedrick (T) Limited, Fredrick Mwakalebela kuhusiana na ushiriki
wa timu katika bonanza hilo na wao wamethibitisha.
Majuto
alisema kuwa kampuni ya Vannedrick (T) Limited ndiyo imeandaa bonanza hilo na
kudhaminiwa na benki ya NMB na wachezaji wake kwa sasa wapo katika
maandalizi ya kina
ili kutwaa ubingwa. Bonanza hilo litaanza saa 2.00
asubuhi.
Alisema
kuwa timu nyingine ambazo zitashiriki katika bonanza hilo ni Barrick, NMB, Dstv
na Radio Times ambazo zipo katika kundi A na Taswa FC pamoja na Jubilee, Azam
Group na wenyeji, Gymkhana wapo katika kundi B.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Vannedrick (T) Limited, Mwakalebela alisema kuwa timu
hizo zitachuano kwa mtindo wa Ligi na timu mbili katika kila kundi zitafuzu
hatua ya nusu fainali na baadaye fainali.
Alisema
kuwa pia kutakuwa na zawadi za mshindi wa tatu mbali ya mshindi wa kwanza na wa
pili. |”Lengo ni kuwaweka pamoja wadau wa michezo ambapo mbali ya kuadhimisha
miaka 51, tutatumia fursa hiyo kujadilia masuala mbaali mbali ya michezo,
matatizo, mafanikio na nini kifanyike,” alisema
Mwakalebela.
Post a Comment