RAIS Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Leodgar Tenga ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo tayari
ametoa notisi ya mkutano huo utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza mapema leo mchana, Ofisa Habari wa TFF,
Boniface Wambura, alisema mkutano huo utafanyika Februari 23 mwakani na
kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini ya
Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Notisi hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao
ni kutoka vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Ajenda za Mkutano Mkuu zitatumwa kwa wajumbe siku 15
kabla ya mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 100.
Post a Comment