Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitoa amri ya
Kuifungia Hoteli ya Giraffe Ocen View iliopo Jijini Dar es Salaam wakati wa
Ziara ya Kutembelea Hoteli zilizopo pembezoni mwa fukwe ya Bahari ya Hindi,
jijini Dar es Salaam.Picha na Ali Meja
---
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –
Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameendelea na ziara ya kikazi ya kukagua hali ya
mazingira katika hoteli zilizopo pembezoni mwa fuke za bahari ya hindi, jijini
Dar es Salaam.
Ziara ya leo imeanzia katika hotel ya Giraffe Ocean View,
na katika hali ya kushangaza maagizo aliyotoa Naibu Waziri Charles Kitwanga
katika hoteli hiyo mapema mwezi huu ya kurekebisha mfumo wa majitaka na kuweka
fukwe katika hali ya usafi hayajazingatiwa.
Hatua kali zimechukuwa wa Hotel hiyo ikiwa ni pamoja na
kufungiwa mpaka hapo itakapotimiza masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria ya
mazingira ya mwaka 2004. “Naifunga Hotel hii ya Girafee mpaka hapo itakapotimiza
masharti ya hifadhi ya mazingira” alilisitiza Dkt.
Huvisa.
Sambamba na hilo Waziri Huvisa ameipongeza Hotel ya Beach
Comber kwa kuwa na mkakati endelevu wa mfumo wa maji taka na hifadhi ya fukwe
kwa ujumla. Dkt. Huvisa amesema kuwa zoezi hilo ni mkakati endelevu wa kukagua
hoteli zote na viwanda, Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira kwa
kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
wanafanya kazi hiyo kwa kikamilifu.
Kwa mujibu wa sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, Hoteli
na Viwanda vyote vilivyoanzishwa kabla ya matumizi ya sheria hiyo vinatakiwa
kufanya (Environmental Audit) na baada ya sheria ya Mazingira hutakiwa kufanya
Tathmini ya Athari za Mazingira (Environmental Impact
Assessment).
Katika ziara ya siku mbili iliyofanywa na Waziri Huvisa
pamoja na Naibu wake Charles Kitwanga imepelekea kuchukua hatua kali za kisheria
ambapo Hotel ya Double Tree na Giraffe Ocean View zimefungiwa mpaka hapo
zitakotimiza masharti waliyopewa.
Na
Lulu
Mussa na Ali Meja
Ofisi
ya Makamu wa Rais
Post a Comment