Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TRENI YA UBUNGO YAIINGIZIA SERIKALI HASARA YA SH. MILIONI 10 KILA BAADA YA SIKU 5

 


MBUNGE wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ametoboa siri kuhusu usafiri wa treni ya masafa mafupi jijini Dar es Salaam, akisema kuwa unaingizia hasara serikali kiasi cha sh milioni 10 kila baada ya siku tano.

Kauli hiyo ilitolewa jijini mwishoni mwa wiki na Mbunge huyo, wakati alipokuwa kwenye ziara ya kichama katika Kata ya Saranga na Kimara.

Mnyika alisema pamoja Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe kujitapa kuwa huduma hiyo inakubalika kwa wananchi, bado haina tija kwa serikali kutokana na hasara hiyo, inayotokana na gharama za uwendeshaji kuwa kubwa.

Alisema mipango ya uanzishwaji ya usafiri huo ilikuwa yaa kurupuka kwani haikuwa na maandlizi ya kutosha haswa katika upande wa miuondombinu ambayo nayo ni sehemu inayoingiza hasara.

“Ninazo nyaraka zinazoonesha mpango mzima wa usafiri huu, ambazo zinaonyesha kuwa bado haujaleta jitija ispokuwa hasara”alisema Mnyika.

Katika hatua nyingine alizungumzia mabilioni ya fedha yaliyofichwa nchini Uswis, Mnyika alisema serikali haipaswi kusubiri wahusika watajwe, kwani watu hao wanafahamika.

Alisema kwani baadhi ya watu waliyofanya hivyo ni miongoni mwa mafisadi waliyotajwa kwenye mkutano uliyofanyika Septemba 15, 2007 kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke.

Mnyika aliitaka serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), chini ya Rais Kikwete, isifanye mzaha kuhusu mabilioni hayo, bali ifanye uchunguzi wa kina na wa haraka kisha iwakamate na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi huo wakutorosha mabilioni hayo.

Aidha, alitoa angalizo kuwa endapo serikali hiyo ya CCM itashindwa kufanya hivyo basi atalizimika kupasua bomu kwa kuwataja wahusika katika bunge lijalo.

Akizungumzia kuhusu kazi za chama, Mnyika alisema kuwa alifanya mikutano 10 kwenye matawi ya kata hizo, ambapo miongoni mwakazi hizo ilikuwa ni kutoa taarifa za utendaji wake wakazi katika kupigania kero zinazo wakabili wananchi wa jimbo hilo.

Pia alizindua vikundi vya wajasiriamali ikiwemo Umoja wa Wanawake Mavurunza Kimaara (Women Group), ambapo katika uzinduzi huo aliendesha harambee kwa ajili ya kutunisha mfuko wa umoja huo.

Katika harambee hiyo, Mnyika alichangia sh milioni 1, huku Wabunge wa Viti Maalumu Naomi Kaihula na Joyce Limo wakichangia sh 500,000 kila mmoja huku jumla ya sh milioni 3.8 zikipatikana katika harambee hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Umoja huo,Blandina Mrutu aliwashukuru viongozi hao, na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa na umoja huo wenye wanachama 15.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top