Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Turkish Airlines yaanza kutumia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro

 


Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines Dkt.Temel Kotl akishuka kwenye ndege ya Turkish Airlines aina ya B737-900 wakati wa hafla uzinduzi wa safari ya ndege hiyo ya Instabul-Kilimanjaro iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mngodo (wanne kushoto) akikata utepe kuzindua safari ya Shrika la Ndege la Turkish Airline kwenye Uwanja wa KIA jana. Watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines Dkt.Temel Kotl.
Baadhi ya abiria wakishuka akishuka kwenye ndege ya Turkish Airlines aina ya B737-900 wakati wa hafla uzinduzi wa safari ya ndege hiyo ya Instabul-Kilimanjaro iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines Dkt.Temel Kotl akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines Dkt.Temel Kotl wakati wa hafla uzinduzi wa safari ya ndege ya Turkish Airlines ya Instabul-Kilimanjaro katika hafla siliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Ndege la Turkish Airlines limeanza rasmi kutumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa safari zake za Instabul-Kilimanjaro – Mombasa kufuatia jitihada za kuboreshwa na kutangaza uwanja huo zinazofanywa na kampuni inayoendesha uwanja huo ya Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO).

Shirika hilo ambalo litafanya safari mara tano kwa wiki liaungana na kampuni za ndege nyingine za Qatar Airways, Qatar ,KLM,Edelweiss Air, Condo Air na Ethiopian Airlines ambayo tayari yamezindua safari zake kupitia uwanja huo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Safari ya Shrika la Ndege la Turkish Airlines kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA jana, Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO Balozi Hassan Kibelloh alisema mvuto wa uwanja huo umetokana na jitihada za makusudi zilizofanya na kampuni yake ilikuufanya uwanja huo kuwa na muonekano wa kimataifa.

“Tunashukuru kwa ujio wa ndege hii ya kimataifa ya Turkish Airlines. Ujio ha ndege hii unatupachangamoto ya kuendelea kuboresha huduma zetu ilituendelee kuvutia ndege nyingine za kimataifa,” alisema.

“Hi ni ishara kuwa Shirika la Turkish Airlines lina imani na uwanja wetu na itatoa fursa nzuri kiushindani. Kutua kwa ndege hii kutaiunganisha Tanzania na nchi nyingine jirani katika masoko yapatikanayo Marekani, Canada na nchi za Ulaya kupitia mtandao mkubwa wa Shirika la Ndege la Turkish.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines Dkt.Temel Kotl wakati wa hafla hiyo alisema kuwa kampuni yake ina imani kubwa na bara la Afrika nakuongeza kuwa wanatarajia kufungua safari nyingine saba kwenye bara la Afrika siku zijazo.

“Tuna imani kubwa na soko liliopo kwenye bara via Afrika na lego letu kubwa kwa sasa ni kuunganisha bara la Afrika na nchi nyingine zaidi duniani. Kwa kuliangalia hilo, tunategemea kuaanzisha safari nyingine saba kwenye Bara la Afrika,” alisema.

Naye Balozi wa Uturuki ncini Ali Davutoglu wakati wa shuguli hiyo alisema nchi yake imesaidia ukuaji wa sekta mbali mbali Barani Afrika zikiwemo elimu, biashara na kilimo.

“Ushirikiano wetu kibiashara na Bara la Afrika unakua kwa kasi sana. Mapato kupitia biashara kati ya Tanzania yamekuwa kutoka dola milioni 18 mwaka 2004 mpaka dola milioni 198 mwishonmi wa mwaka 2011,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana