Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MKUU AHIMIZA MAZAO MBADALA YA BIASHARA


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wakazi wa wilaya mpya ya Mlele
mkoani Katavi walime mazao mbadala ya biashara kama alizeti, karanga
na ufuta kwa sababu yanachukua muda mfupi na hivyo kuleta kipato cha
haraka.
Ametoa wito huo juzi jioni (Ijumaa, Desemba 14, 2012), wakati
akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nsenkwa mara baada ya kuweka jiwe
la msingi kwenye zahanati ya kijiji hicho akiwa katika siku ya pili ya
ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao kuachana na mazoea ya kulima tumbaku
kwa vile inachukua muda mrefu hadi kukomaa na inachangia uharibifu
mkubwa wa mazingira kwani inahitaji kuni nyingi wakati wa kukausha.
“Tumbaku hivi sasa haina bei kwa sababu wanaopanga bei ni wakubwa huko
nje… tuangalie mazao ya alizeti, ufuta na karanga kwa sababu yanatoa
pesa kwa haraka zaidi. Mfano mzuri ni Singida ambao wamekuja juu
kiuchumi kwa sababu ya zao la alizeti,” alisisitiza.
Aliwataka wakazi hao waangalie ufugaji nyuki kama fursa ya kipekee kwa
sababu mkoa huo umejaliwa kuwa na misitu mingi na unaweza kuongeza
kipato cha mkoa wao. “Asali ni dawa, asali ni chakula, asali ni
biashara na ina soko hapa nchini hadi nje ya nchi. Changamkieni fursa
hii, ongezeni uzalishaji wa asali na nta,” aliongeza.
Aliwashauri pia waangalie uwezekano wa kulima miembe ya kisasa kwa
sababu inazaa kwa wingi na katika kipindi kifupi mno. “Hii miembe yenu
inazaa maembe 10-20 kwa mwaka lakini ya kisasa inazaa hadi maembe
10,000, ikiwa chinichini tu,” alisema.

Akihimiza kanuni bora za kilimo, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo
la Mlele aliwataka waachane na kilimo cha matuta na badala yake
watumie kilimo cha sesa. “Ekari moja ya mahindi inapaswa ikupatie
magunia 20-25 ya mahindi, sasa wewe unalima ekari tatu na kuvuna
magunia 10, sababu kubwa ni nafasi zinazopotea kwenye miraba ya
matuta, alisema.
“Ni lazima tuondokane na kilimo hiki kwa sababu hakina tija na tena
kinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo lingetumika
kupanda mazao,” alisisitiza.


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top