Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wizara Ya Afya Kuanzisha Kinga Ya Kuzuia Vifo Kwa Watoto

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii inatarajia mwaka ujao kuanzisha chanjo mpya mbili za Pneumococcal na Rotavirus, ambazo ni maalum katika kukinga maradhi na vifo kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam leo, na Mkurugenzi wa Kinga, Elias Chinamo, wakati wa warsha ya siku moja ya wandishi wa habari, ya kuwajengea uwezo wa kufilisha elimu sahii kwa jamii pamoja na kuihamasisha jamii kuhusu chanjo hizo mpya, zitakapoanza mwaka 2013.

Alisema walengwa wa chanjo hizo watakuwa ni watoto waliyonaumri wa chini ya miezi 12 ambapo chanjo ya kukinga nimonia (pcv13), itatolewa mara tatu kuanzia umri wa wiku sita, 10 na 14.
Chinamo akubainasha kuwa chanjo ya kinga ya kihara (rotavirus), itatolewa mara mbili kuanzia imri wa wiku sita na 10, inasisitizwa kuwa ili mtoto apate kinga lamili ni lazima akamilishiweratiba mapema.

Alisema kitaalam zinaonesha kuwa chanjo ya ‘Pneumococcal’ hukinga maambukizi ya nimonia kwa asilimia 38, homa ya uti wa mgongo kwa takriban asilimia 87; na chanjo ya ‘rotavirus’ hukinga kuharisha kuharisha kunakosababisha vifo vya watoto kwa aslimia 80.
Chinamo aliongeza kuwa kwa sehemu kubwa hukinga ugonjwa wa kuharisha unaosababshwa na vimelea vya aina nyungune pia.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top