Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

YALIYOJILI KWENYE TASNIA YA FILAMU MWAKA 2012.

 
MWAKA ndio unakatika katika tasnia ya filamu kuna mengi yalitokea na kuandikwa kutoka kwa wasanii wa filamu Bongo ikiwa wasanii waliongoza kwa mauzo ikiwa ni mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu, huzuni nayo kwa mwaka huu ilitawala katika sekta hiyo inayoshika kasi nchini kwa kuzalisha filamu nyingi.

.
Yvonne Cherryl
Monalisa nyota ing'arayo Swahiliwood.
SAFARI
Msanii Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ na marehemu Steve Kanumba waliweza kusafiri kikazi kwenda nchini Ghana kwa ajili ya kufanya usahili kwa ajili ya kushiriki katika filamu ambayo ilishirikisha wasanii nyota kutoka Nijeria, Ghana, Afrika ya Kusini na nchi zingine, katika safari hiyo pia wasanii kama Rose Ndauka na Lucy Komba nao walisafiri kwa ya kwenda kujaribu bahati yao ambapo mwanadada Lucy Komba alipata nafasi ya kuingia mkataba wa kurekodi filamu ya ESCAPE TO AFRICA (Repackaged lives).


Filamu zilizofanya vizuri.

Filamu zilizotikisa na kuuzwa sana ilikuwa ni filamu Tax Driva ya JB, Principle of Women ya Ray, Nakwenda kwa Mwanangu, Pastor Myamba The Trial, Ndoa Yangu kati ya filamu zilizoachwa na marehemu ni filamu iliyosubiriwa na wapenzi wa filamu kwa hamu, huku filamu ya Chungu iliyotengenezwa na msomi kutoka Chuo kikuu Dar es Salaam Dr. Vicensia Shule ikiibuka filamu Bora kwa mwaka 2012 katika tuzo za Zanzibar International Film Festival (ZIFF).
.

Jacob Stephen
JB mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.
Jaqueline Wolper
Jack Wolper msanii wa filamu.
VIFO.
Misiba ilitikisa kwa mwaka huu kwani mwezi wa April msanii nguli katika tasnia ya filamu Swahiliwood Steven Kanumba alifariki Dunia baada ya kujigonga katika tendegu la kitanda ikidaiwa kusukumwa na msanii mwezake Elizabeth Michael ‘Lulu’ msiba huu ulizua hisia za watanzania na kuandika historia nchini kwa msanii huyo kuzikwa na mamia ya watu huku kila kiongozi akihudhuria msiba huu.

Vifo viliendelea ambapo msanii mkongwe katika maigizo na filamu Mlopelo alifariki, wiki hiyo hiyo msanii John Maganga naye alifariki baada ya kuugua na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyala na baadae kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, huzuni zilizidi kutawala pale msanii nyota wa vichekesho na muziki Sharomilionea alipopata ajali mbaya ya gari eneo la Maguzuni Mkoani Tanga, msanii pia naye aliandika Historia katika kijiji alichozaliwa cha Lusanga kuzikwa na mamia ya watu ambayo haijawahi kutokea katika mkoa wa Tanga na si kijijini Lusanga tu.
MAHUSIANO.
Mahusiano nayo yalishika kasi kwa wasanii huku tukishuhudia wasanii wakibadilisha Dini baada ya kupata mapedejee na kutangaza uhusiano wao kwa mbwembwe wasanii walioandikwa sana katika hilo alikuwa na Jack Wolper aliyetangaza kuolewa na Dallas, lakini hatimaye ndoa iliota mbawa, huku Aunty Ezekiel akiingia katika mkumbo huo na kufanikisha jambo la ndoa baada ya kufunga ndoa umangani na Sunday, huku msanii Rose Ndauka akibadili Dini kwa ajili ya Ndoa ambayo hadi leo haijafungwa akiishi na Marik bila Ndoa..

MARADHI.
Msimu tasnia ilikumbwa na mikasa ya wasanii kuugua msanii Sajuki ambaye alipata maradhi ya uvimbe tumboni na kuhitaji matibabu nje ya nchi na kusafirishwa India baada ya watanzania kumchangia kufanikiwa kusafiri alipata matibabu hata hivyo pia inampasa kurudi India kuendelea na matibabu ambayo ni gharama, msanii mkongwe Said Wagamba ‘Mzee Small naye anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi pamoja Mzee Kangaa tunawaombea Mungu awaponye haraka.

MIKASA.
Kuna baadhi ya wasanii hasa wa Kike waliandamwa na kashifa na kuandikwa sana jambo ambalo liliwaradhimu kuomba msamaha wasanii hao ni Aunty Ezekiel, Wema Sepetu waliovuma kwa kupigwa picha katika majukwaa ya matamasha wakiwa nusu uchi na baadae kuomba msamaha kwa jamii baada ya mkwara wa TAFF na BASATA, huku Rayuu yeye akikumbwa na kashifa ya kujipiga picha ya nusu uchi na kusambaza katika mitandao nao wanalo la kujitia.

Serikali ilitangaza kuitambua tasnia ya filamu kuwa ni sekta rasmi na kutangaza kuwa mwaka ujao mamlaka ya Mapato (TRA) itaingia rasmi kwa ajili ya kweka alama ya utambulisho katika harakati ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii kwa kushirikiana taasisi husika.
Mikasa haikuishia hapo kwani kwa mara ya kwanza wanawake katika tasnia ya filamu kwa mwaka huu ilikuwa ni mwaka wao kwa kila jambo la kuumiza pale mabinti wawili wakiwa lupango hadi leo kwa kesi tofauti ambao ni Elizabeth Michael ‘Lulu’ akituhumiwa kwa kesi ya kusababisha kifo cha msanii mwenzake marehemu Kanumba, naye binti Kajala Masanja akiwa Segerea kwa kesi ya kutakatisha fedha za Takakuru na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.
.

Single Mtambalike-+
Richie akiwa katika pozi.
Juma Kilowoko
Sajuki msanii wa filamu Swahiliwod.
WALIONG’ARA.
Kwa mwaka huu unavyoongelea wasanii walioshika katika tasnia ya filamu kwa upande wa wanaume nambari moja JB, Steven Kanumba, Hisany Muya ‘Tino’ msanii chipukizi Slim Mrisho, Baga, Kapturado, Yusuf Mlela, Hemed Suleiman, Richie, Richard Mshanga ‘Mzee Masinde’ ambaye ndio mwigizaji bora wa Kiume tuzo za ZIFF mwaka 2012, huku wasanii wasiotabirika kama Ray wakiendelea kufanya vizuri.

Kwa upande wa kina dada kama kawaida msanii asipotea katika game Monalisa alikuwa kinara Jack Wolper aliwafunika wenzake, Jenifer Kyaka ‘Odama’ Mariam Ismail, Riyama Ali bado nyota yake inaendelea kuwaka, Aunty Ezekiel naye hakuwa nyuma huku Wema Sepetu akifanya vizuri Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliongelewa kwa mwaka huu, pia kuna wale wasanii wenye mvuto hata bila kufanya kazi nyingine bado uongelewa basi hapa unakutana na mwanadada nyota Irene Uwoya pia unakutana Shilole anayejiongezea umaarufu kwa kukata viuno stejini.
KING MAJUTO.
Msanii mkongwe Amri Athuman ‘King Majuto’ alishindwa kuficha hisia zake kwa kifo cha meneja wake aliyepoteza maisha katika ajali ya gari Sharo milionea alipozimia mara kadhaa huku akisema kuwa kukutana na sharo milionea kwa muda mfupi alibaini thamani yake na kufanikiwa kuingia mikataba minono ya matangazo.
.

Amri Athuman
King Majuto mchekeshaji Bongo.
Mwisho ni wiki kadhaa tu ambapo tena tasnia ya filamu ilikumbwa na kadhia nyingine pale msanii mkongwe na mahiri katika filamu Hidaya Njaidi alipopata ajali mbaya maeneo ya Mabibo baada ya kupindukia na gari aina ya Noah akiwa anaelekea katika sherehe za Kitchen Party Maeneo ya Mbezi beach, msanii alipata majeraha mwilini ikiwa pamoja mkono wake kuumia sana na kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Moi ambako anaendelea na matibabu.
Mwaka huu mgumu wa wasanii na wadau wa tasnia ya filamu soko likiendelea kusuasua wasanii wakiongezeka kila kukicha hiyo ni dallili kuwa suala la ajira Bongo bado ni kitendawili.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top