Wachezaji
wa Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao,
Ismail Dunga
kulia
MABINGWA wa Kenya, Tusker
FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
katika mchezo wa kirafiki jioni hii.
Huo ulikuwa mchezo maalum
kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari ya Uturuki Jumamosi usiku
kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.
Hadi mapumziko, Tusker
walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani na kiungo Ismail
Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44.
Refa Charles Oden Mbaga
alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari kumuangusha kwenye
eneo la hatari, kiungo Khalid Aucho.
Yanga walicheza vema katika
kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza nafasi za kufunga na hilo
lilitokana na mipango haba ya safu yake ya kiungo leo, ikiongozwa na Kabange
Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja na kocha Mholanzi
Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza Hamisi Kiiza,
Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar Khalfan kuchukuwa nafasi za akina
David Luhende, Said Bahanuzi, George Banda, Rehani Kibingu na Oscar Joshua,
lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi Yanga iliongeza kasi
ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata Nizar alipoingia, lakini kwa
ujumla bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Hii ni mechi ya pili
Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga tangu aanze kazi akirithi
mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine saba ameshinda na moja ametoa
sare.
Yanga SC; Ally Mustafa
‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo,
Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange Twite, George Banda, Said Bahanuzi na
David Luhende.
Tusker FC; George Opiyo,
Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho,
Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk
![]() |
Wachezaji
wa Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao, Ismail Dunga kulia |

Post a Comment