African
Lyon ndiyo klabu iliyoongoza kwa kusajili wachezaji wengi kwenye dirisha dogo
kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaotoa bingwa wa
Tanzania Bara, lakini pia timu tatu ambazo msimu ujao zitarudi kucheza Ligi
Daraja la Kwanza.
Kati ya
wachezaji 65 waliotua katika klabu mbalimbali katika dirisha hilo, Lyon ndiyo
iliyoongoza kwa kuwanasa 12. Miongoni mwao hao, wawili (Ibrahim Job na Shamte
Ally) imewachukua kwa mkopo kutoka Yanga.
Pia watano imewapandisha kutoka
katika kikosi chake cha U 20. Wachezaji hao ni Nurdin Musa, Salvatory Jackson,
Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na jarufu Kizombi. Wengine walioingia katika
timu hiyo katika dirisha dogo ni Juma Seif (Huru), Buya Jamwaka (Burkina Faso),
Takang Valentine (Huru) na Yusuf Mgwao (Huru).
Nayo
Polisi Morogoro katika kuhakikisha inaondoka mkiani mwa ligi imesajili wachezaji
wanane katika dirisha dogo kama ilivyofanya Oljoro JKT ya
Arusha.
Wachezaji
wa kigeni walioingia katika dirisha dogo ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins
Atudo (Azam), Donald Obimma na Ulugbe Chika (Toto Africans), Zuberi Hamis na
Tinashe Machemedze (Coastal Union), Musa Mudde na Abel Dhaila
(Simba).
Post a Comment