picha na
maktaba
Vurugu kubwa zinaendelea
hivi sasa eneo la Dumila mkoani Morogoro, kufuatia wananchi kufunga barabara ya
Morogoro Dodoma, kwa kile wanachodai kumtaka Mkuu wa Mkoa Joel Bendera kufika
kuwatatulia tatizo lao la kunyang'anywa maeneo yao ya wakulima na kuwapatia
wafugaji.
Wananchi hao wamegawanyika
katika makundi kadhaa huku kila kundi likifunga barabara ya kuingia na kutoka
eneo hilo la Dumila, ambapo wamezuia magari yote yanayopita eneo hilo kutoka
moro na kotoka Dom, huku wakichoma magaro na kuvunja vioo vya magari hovyo,
pamoja na kuchoma moto nyumba za wageni na kuvunja vioo.
Tayari Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, ameomba udhuru kutoka katika Kikao cha wakuu wa mikoa, kilichokuwa
kikiendelea mkoani Dodoma, na hivi sasa yupo njiani akielekea eneo hilo kwa nia
ya kukutana na wananchi hao ili kuwasikiliza na kutatua mgogoro
huo.
Mtandao huu utaendeleo
kuwajuza kinachoendelea kadri habari zitakavyopatikana
Post a Comment