SHIRIKA la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Wings of Kilimanjaro ya nchini
Australia, wameandaa safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro itakayowashirikisha
watalii zaidi ya 100 ambao watashuka toka kwenye kilele cha mlima huo kwa
kutumia miavuli maalumu.
Aidha, shughuli hiyo
inayotarajiwa kukusanya dola milioni moja (sh bilioni 1.5) ambazo zitatumika
kusaidia miradi ya wananchi wanaoishi kuzunguka hifadhi mbalimbali za taifa
nchini.
Wakizungumza na
waandishi wa habari jijini hapa juzi, Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal
Shelutete na Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Adrian Mgrae, walisema fedha hizo
zitaelekezwa kwenye miradi mbalimbali ya kukabiliana na umaskini vijijini,
uharibifu wa mazingira na misaada ya kibinadamu.
Walisema misaada hiyo
inajumuisha uchimbaji wa visima vya majisafi ya kunywa, kuboresha miundombinu ya
elimu na kusaidia waathirika wa ukimwi, ikisimamiwa na mashirika yasiyo ya
kiserikali ya One Foundation, Plant with Purpose na Worldsave International
Post a Comment