Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania
Hair Industry ltd James Walwa - Jimmy akimkabidhi mbunifu wa mavazi
nchini Ally Rehmtullah tiketi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Afrika
Mashariki katika mkutano wa 'The Economics of the Africa Fashion
Industry' utakaofanyika nchini Marekani mwezi wa Februari. Tanzania
Hair Industry ltd ambao ndio watengenezaji wa nywele maarufu aina ya
Darling ndio wadhamini wa safari ya mbunifu huyu kwenye mkutano huo wa
kihistoria utakaofanyika katika Kikuu cha Havard nchini Marekani.
---
Mbunifu mahiri wa mavazi
nchini Tanzania Ally Remtullah amechaguliwa kuiwakilisha Africa
Mashariki katika ‘East Africa Fashion Industry’ kuongea katika
mkusanyiko wa Afrika Business Conference utakaofanyika Harvard Business
School nchini Marekani.
Akizungumza na Mo Blog
jijini Dar es Salaam leo, Mbunifu huyo Remtullah amesema shughuli hiyo
itakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Marekani cha Harvard ambacho ni
kikubwa kuliko vyote duniani itafanyika Februari tarehe 15 mwaka 2013.
Akifafanua amesema kuwa
kila mwaka Chuoni hapo kunafanyika mikutano ya ‘Africa Business
Conference’ ikiwa na kauli mbiu tofauti na sasa mwaka huu yeye
amechaguliwa kuwa mmoja wa wazungumzaji kuhusiana na ‘The Economic of
Africa Fashion’.
Ally Remtullah amesema kwa
ujumla anaiwakilisha Afrika Mashariki katika kategori hiyo ambapo
anatarajiwa kuzungumzia changamoto zinazoikabili na fursa zinazopatikana
katika tasnia ya fasheni Afrika Mashariki, ikiwemo tatizo la umeme na
gharama za manunuzi ya vitambaa vya Pamba ambayo kimsingi huzalisha
katika ukanda huu.
Amesema anafurahi
kuchaguliwa na wandaaji hao kuziwakilisha nchi za Afrika Mashariki na
sasa si kwenda tena kuonyesha mavazi, bali ni kuzungumza mbele ya wadau
wakubwa wa kidunia kuhusu nafasi ya masuala ya ubunifu na uchumi.
Wazungumzaji wengine katika mkutano huo ni pamoja na mbunifu maarufu wa Afrika Magharibi Ituen Basi kutoka Nigeria.
Katika maandalizi hayo
Ally amesema pamoja na kusoma vitu vingi kuhusiana na uchumi katika
tasnia ya fasheni na gharama za uzalishaji za viwanda vya nguo, pia
amekutana na wafanyabiashara wakubwa wa viwanda vya kutengeneza nguo
hasa za kiafrika akiwemo Mfanyabiashara Mkubwa nchini Mh. Mohammed Dewji
ambaye kwa namna moja ama nyingine amempa ushirikiano wa kutosha.
Safari hiyo ya mbunifu wa
mavazi nchini Ally Remtullah katika mkutano mkubwa wa kihistoria wa
Boston nchini Marekani, imedhaminiwa na kampuni ya Tanzania Hair
Industry Ltd, ambao ni wazalishaji wa nywele maafuru aina ya Darling.
Post a Comment