|
Wazee
kumi kutoka Mkoani Mtwara wakiwa wanaingia kwenye ukimbi wa Mikutano wa
Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakiwawakilisha wanamtwara kwa ajili
ya kuja kutoa Tamko lao kuhusiana na Gesi iliyoundulika Mkoani kwao.
Miongoni mwa wazee hao wamesema kuwa wamelazimika kuuza Mifugo yao ili
kupata nauli ya kuja Dar es Salaam. |
|
Hawa ndio wazee kumi kutoka Mtwara wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Habari maelezo jijini Dar es Salaam |
|
Mzee Selemani Mademu akisoma Tamko kwa niaba ya wenzake
Wazee
wa Mtwara Mikindani leo wameongea na waandishi wa habari kataika ukumbi
wa habari Maelezo kuelezea matakwa yao kwa Serikali juu ya Swala zima
la Gesi ambayo inapatikana katika Mkoa wao.
Akizungumza
kwa niaba ya wazee wenzake Mzee Selemani Mademu amesema kuwa wanaitaka
Serikali kuhakikisha kuwa Gesi inawafaidisha wao kwanza kabla ya kwenda
kuwafaidisha wengine.
Amesema
kuwa wao wametumia Gharama zao wenyewe ikiwa ni pamoja na kuuza Mbuzi
wao ili wapate nauli ya kuja kuitetea Gesi yao kwa manufaa ya wanamtwara
wote kwa Ujumla.
Ameendelea
kusema kuwa, wanaitaka serikali ihakikishe kuwa kituo cha kusafishia
Gesi kinajengwa mkoani Mtwara kwani kuna bandari yenye kina kirefu kwa
ajili ya Kazi hiyo na amesema kuwa wanaitaka serikali katika
kutekeleza swala hilo ifanye vitendo kwanza na sio ahadi kama
ilivyozoeleka.
“Tumechoshwa
na ahadi za Serikali na kwa hili hatuhitaji tena ahadi tunataka vitendo
la sivyo Gesi haitoki Mtwara tutazidi kuandamana, tuna rekodi ya ahadi
tuloyo ahidiwa na Serikali na hazijatekelezwa mpaka leo kama vile:
Barabara, Umeme, kuimarishwa kwa Bandari, Mikopo kwa ajaili ya
Ujasiriamali, viwanda vidogo kwa ajili ya Kubangua korosho n.k kwa
hivyo sisi tunataka vitendo tu, tushachoshwa na ahadi”, amesema Mademu.
Serikali
pia imetakiwa, kutimiza ahadi ya kujenga viwanda kama vya Mbolea na
Saruji kama ilivyo ahidi kwa wanaMtwara jambo ambalo litawapa
Matumaini yasiyokuwa na Shaka kuhusu kupata Ajira, pamoja na kuratibu
mchakato mzima wa Matumizi ya Gesi kwa kuwashirikisha mikoa ya kusini
kwa hatua Zote na kwa uwazi.
Aidha wameitaka Serikali kujenga kituo cha kufua Umeme Power Plant Mtwara.
Wazee hao
pia wamekanusha taarifa za Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe, James Mbatia
za kuwa alishushwa Jukwaani tarehe 13/01/2013 na kusema kuwa jambo hilo
halina ukweli wowote.
| | | | |
on Wednesday, January 23, 2013
Post a Comment