Asha
Baraka
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya The African Stars, Twanga Pepeta,Asha Baraka, amewataka wanamuziki na wamiliki wa bendi kuwachukua wanamuziki wao chipukizi kutoka Twanga Academy, kwa kufuata taratibu ili wasitokee wa kuwarubuni vijana hao wadogo kimuziki.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Asha alisema amegundua kuna baadhi ya wanamuziki wameanza kupita chini chini kuwarubuni vijana wao bila kufuata utaratibu, ili wasiuwe vipaji vyao.
Alisema wameamua kuanzisha Academy hiyo ili kuibua vipaji vipya, hivyo mtu yoyote mwenye mipango ana uwezo wa kuwachukua vijana hao na kuwaendeleza zaidi, baada ya kuibuliwa.
"Leo hii kama mtu anakuja na kuzungumza na chipukizi kutoka kwetu kienyeji, hatuwezi kuchekea suala hilo, hivyo watu wafuate utaratibu.
"Naamini katika hili jamii nzima itanielewa, hivyo naomba wanamuziki na wamiliki wa bendi wawe wawazi kwa ajili ya kukuza muziki wa dansi," alisema Asha.
Ingawa Asha hakuwataja vijana wanaotaka kuchukuliwa kienyeji, lakini ubora wa Twanga Academy, umeanza kuleta hisia kuwa baadhi yao wanaweza kufika mbali, endapo wataongeza bidii.

Post a Comment