KWA
UFUPI
ATCL
ilisitisha safari zake April 9, 2012 baada ya ndege yake aina ya Dash 8 kupata
ajali katika kiwanja cha Kigoma, hivyo Shirika hilo kukosa ndege nyingine. Miezi
miwili iliyopita shirika hilo lilinunua ndege mpya.
ABIRIA 25 waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la
Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam wamenusurika kufa baada
ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata ufa katika kioo cha mbele, hivyo kumfanya
rubani abadili mwelekeo na kutua kwa dharura uwanja wa ndege wa
Kigoma.
Tukio hilo lilitokea juzi jioni muda mfupi baada ya
ndege hiyo aina ya Bombadia Dash 8 kuruka katika uwanja wa ndege wa Kigoma,
ikiwa katika safari zake za kwanza, baada ya kusitishwa takriban miezi tisa
iliyopita.
ATCL ilisitisha safari zake April 9, 2012 baada ya
ndege yake aina ya Dash 8 kupata ajali katika kiwanja cha Kigoma, hivyo Shirika
hilo kukosa ndege nyingine. Miezi miwili iliyopita shirika hilo lilinunua ndege
mpya.
Kaimu Mkurugenzi wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro alisema
ilipata hitilafu hiyo dakika 15 tangu iliporuka, baada ya kioo cha mbele kupata
ufa.“Ufa ule uliwatisha marubani na waliamua kutua kwa dharura kwa sababu kioo
kingeweza kupasuka na kusababisha ajali mbaya na ndege kuanguka,” alisema Lazaro
na kuongeza;
“Kawaida vioo vya ndege hupashwa moto ndege inapoondoka
na endapo utatokea ufa wowote ni lazima irudi kiwanjani na kama ipo mbali na
kiwanja inambidi rubani ateremke chini na kupunguza mwendo.”
Alisema kutokana na hali hiyo, wapo kwenye harakati ya
kuifanyia matengenezo ndege hiyo na wakati wowote itarudi kwenye safari zake za
kawaida.
Post a Comment