Mbali na kupiga picha
hiyo na Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, kijana huyo
alionekana katika picha hiyo akionyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya
Chadema.
Hata hivyo, baada
ya picha hiyo, JWTZ lilimtilia shaka kijana huyo na kutangaza rasmi kumsaka, ili
lijiridhishe kama ni mmoja wa wanajeshi wake.
Baada ya kumsaka
kwa takriban siku 12, kijana huyo alikamatwa Januari 3, katika Mji wa
Bomang’ombe wilayani Hai na baada ya kupekuliwa alikutwa na sare
hizo.
Jana, Kikulu
alifikishwa mahakamani mjini Moshi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kusomewa
mashtaka mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya kama ilivyodaiwa
mahakamani.
Baada ya kukiri
kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, alimhukumu
kifungo cha miaka minne jela, ili iwe fundisho wa wakosaji wengine wa aina
hiyo.
Kabla ya hukumu
hiyo, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alimsomea mshtakiwa huyo mashitaka yake
mawili, likiwamo la kujifanya Ofisa wa Jeshi, wakati akijua ni
uongo.
Wakili huyo
alidai mahakamani kuwa Januari 3, mwaka huu katika eneo la Bomang’ombe wilayani
Hai, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama mtumishi wa
umma.
Katika shtaka la
pili, wakili huyo alidai siku hiyo hiyo katika Mtaa wa Msikitini, eneo hilo la
Bomang’ombe, mtuhumiwa alipatikana na sare za JWTZ kinyume cha
sheria.
Sare hizo ni
pamoja na suruali moja, mashati mawili na kofia mbili, vyote vikiwa na alama za
Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Baada ya Hakimu
Kobelo kumuuliza mshtakiwa kama ni kweli alitenda makosa anayoshitakiwa,
mshtakiwa huyo alikiri makosa yake katika hali ambayo
haikutarajiwa.
Kutokana na
kukiri kwake makosa hayo, Hakimu Kobelo alimhukumu kifungo cha miaka miwili kwa
kosa la kwanza la kujifanya Ofisa wa JWTZ na miaka mingine miwili kwa kosa la
pili.
Hata hivyo,
Hakimu Kobelo alisema kuwa kwa kuwa adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja
(concurrent), mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka miwili
jela.
Kwa mujibu wa
hakimu huyo, kosa alilolifanya mtuhumiwa huyo ni baya na linastahili adhabu
kali, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya sare za majeshi
nchini.
Mwananchi
Post a Comment